Kijana aliyewezeshwa na Airtel FURSA aweza kutoa ajira kwa vijana wengine 15 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kijana aliyewezeshwa na Airtel FURSA aweza kutoa ajira kwa vijana wengine 15



 Mwanza, Mafanikio ya Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuhakikisha Kijana  mkulima mdogo aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel  FURSA Tunakuwezesha ameweza kuongeza ukubwa wa shamba, mazao na kuajiri wengine yameanza kuonekana baada ya mkulima mdogo Innocent Kipondya wa  kijiji cha Mwalogwabagole wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuajiri  vijana wenzake 15 shambani kwake. 


Kupata mafanikio kwa Innocent kunafuatia miezi 11 iliyopita Airtel FURSA
kumwezesha pampu ya kuvuta maji na mpira wake, ikiwa ni pamoja na bajaji kwa ajili ya kusafirisha mazao sokoni.

Innocent amesema ilikuwa inampa wakati mgumu kulima wakati wa kiangazi lakini sasa anaweza  kulima wakati wote kwa kumwagilia kutokana na pampu ya kuvuja maji  aliyowezeshwa na Airtel FURSA.

“ Kabla sijashikwa mkono na  Airtel Fursa nilikuwa napata changamoto ya mazao kukauka kutokana na  maji kuwa mbali, lakini sasa licha ya kupanua kilimo, nina uhakika wa  kulima mwaka mzima” amesema Innocent

Innocent amemwambia mwandishi wa habari hii kuwa, soko la nyanya ni la uhakika na sasa  ameamua kulima mbogamboga na kupanua kilimo cha mpunga, japo kuwa wadudu waharibifu ni kikwazo kwake kupata mazao mengi zaidi. Ameipongeza


Airtel kwa kuwajali vijana hapa nchini, na sasa amefanikiwa kusimamisha
jengo na baadaye ana mpango wa kununua wanyama kazi kwa ajili ya
kulima.

Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael  ,mbali na kumpogeza Innocent kwa bidii aliyoionyesha alipomtembelea,  amesema dhana ya kampuni yake ni kuendelea kuinua vijana na  wajasiliamali wadogo hapa nchini ili kuweza kubadilisha maisha yao.

“Miezi 11 nilikuja hapa, shamba la nyanya lilikuwa moja tu,lakini sasa naona
mashamba manne,bustani ya mbogamboga,kilimo cha mpunga hata vitungu,nampongeza sana Innocent” aliongeza Emmanuel

Airtel  Fursa ni mradi wa kijamii wenye lengo la kuhamasisha vijana, kuwapa  fursa ya kujiendeleza kibiashara na kuwapa ujuzi utakoawawezesha  kuimarisha biashara zao katika mikoa yote nchini .

Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akimuonyesha Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael mazao aliyepota baada ya kuwezeshwa, alipotembelewa shambani kwake hapo jana.
Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akibeba mazao aliyofuna baada ya kuwezeshwa miezi 11 iliyopita.

Kijana Innocent Kipondya (juu ya Toyo) aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akiwa anaelekea sokoni baada ya kuvuna mazao yako na kupata faida na kuweza kuajiri vijana wengine 15.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages