Nae Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema kuwepo kwa huduma za kibenki kupitia mitandao ya simu kumewezesha wateja wao kupata huduma kirahisi tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kuanza kwa huduma ya mobile banking.

Alisema kupitia huduma hiyo kwa sasa wateja wao wanauwezo wa kutoa fedha, kulipia huduma mbalimbali kama kodi, kununua umeme, tiketi za ndege na hata kuangalia salio lililo katika akaunti zao za benki na wanachokifanya kwa sasa ni kuangalia jinsi gani wanaboresha zaidi huduma hizo kwa wateja hasa walio maeneo ya vijijini.

“Miaka ya nyuma kama mteja yupo kijijini anatumia muda mwingi kwenda sehemu iliyo na huduma ya benki lakini kwa sasa huduma za kibenki katika mitandao ya simu imerahisisha hata wateja wetu walio vijijini kupata huduma zetu kiurahisi,” amesema Bi. Bussemaker.

 Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumza katika mkutano huo.

Nae Meneja wa Mifumo wa Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi amesema huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu imekuwa ikizidi kukua siku baada ya siku tangu ilipoanza nchini mwaka 2008 na mpaka sasa kuna benki 30 ambazo zimejiunga katika mfumo huo ili kuwasogezea huduma wateja wake.