Pages

PAPA FRANCIS AWACHUKUA WAKIMBIZI 12 NA KUWAKARIBISHA KUISHI ROMA

Papa Francis leo amewakaribisha wakimbizi 12 wa Syria wakati wakiwasili Jijini Roma baada ya kuwachukua kutoka kwenye kambi ya Lesbos kufuatia ziara yake katika kisiwa hicho cha Ugiriki.
Familia tatu za wakimbizi wa Syria walipanda ndege ya Papa Francis punde tu baada ya ziara yake hiyo ya Lesbos kuangazia mgogoro wa kibinadamu unaotokana na wakimbizi.
                 Papa Francis akiwakaribisha wakimbizi wa Syria aliowachukua Lesbos

Msemaji wa Vatican amesema Papa Francis ameamua kuonyesha ishara ya kuwakaribisha wakimbizi hao kwa kuwachukua kukaa Roma ambao miongoni mwao wamo watoto sita.

              Papa Francis akimbusu mtoto mkimbizi wakati wa ziara yake ya Lesbos

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)