Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi Jeshini waliagwa.
Brigedia Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya kumaliza utumishi wao jeshini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, akikagua gwaride hilo.
Wanafamilia wa wastaafu hao wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuagwa jamaa zao.
Ukaguaji gwaride rasmi ukiendelea.
Maofisa hao wastaafu wakiwa jukwaa kuu.
Hapa maofisa hao wakiwa wamesimama wakati gwaride likipita jukwaa kuu na kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo.
Askari wa JWTZ wakifuatia matukio mbalimbali kwenye
hafla hiyo.
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba, akikagua gwaride hilo maalumu kwa ajili ya kuagwa.
Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo mstaafu, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
Wapiga picha wa magazeti wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali.
Taswira ya jukwaa kuu katika hafla hiyo.
Wastaafu hao wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi.
Mkuu wa majeshi, Davis Mwamunyange (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi wastaafu. Kushoto Robert Mboma na George Waitara (kulia).
Mkuu wa majeshi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
Hapa ni furaha tupu kwa kustaafu utumishi ndani ya jeshi.
Askari wa JWTZ wakiwa imara wakati wa kuwaaga maofisa hao.
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam.
Hapa ni saluti wakati wakiwaaga wapiganaji wenzao.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba.
Tukio la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu utumisho wao jeshini limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Hafla hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi hilo.
Majenerali hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine.
Majenerali hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wengine ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur nchini Sudani.
Kwa upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.
Wengine ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Chalres Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Mhunga.
Na wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi , Mkuu Tawi la Ukaguzi jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
Wengine ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah , Mkuu wa Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia Jenerali Ezra Ndimugwango.
Na wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya 'Eflantria' mkoani Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.
Akizungumza mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)