Pages

RAIS KABILA AWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA KWA KUTWAA UBINGWA WA CHAN 2016

 Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) akiwa amebeba kombe la ubingwa wa CHAN2016 katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya nchi hiyo 'Leopards' Ikulu ya Kinshasa mwishoni mwa juma ambapo alimzawadia kila mchezaji gari aina ya Prado. Pamoja na magari Rais Kabila pia alimpa kila mchezaji Medali maalum ya Kutukuka katika michezo (Sporting Merit). Yote hii ni baada ya kuichapa Mali bao 3-0 Jumapili katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ambayo ni kwa wachezaji wa ligi za ndani barani Afrika. Mwaka 2009 DRC walichukua kombe hilo pia wakati wa kuanza kwa michuano hiyo.
 Sehemu ya magari waliyozawadiwa wachezaji wa Timu ya Taifa ta DRC 'Leopards' baada ya kunyakua kombe la CHAN2016

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)