Pages

Vitus Mhusi:Kutoka kwenye maabara hadi Meneja wa kiwanda

 Vitus akiwa ofisini kwake
 Vitus akiwa nje ya jengo la kiwanda cha TBL cha Moshi
Vitus akiangalia Shahiri moja ya malighafi inayotumika kutengenezea bia
Asema mafanikio yoyote yanatokana na kufanya kazi kwa bidii
Ukifika katika kiwanda cha TBL cha Moshi ambacho kinatengeneza malighafi za kutengenezea bia kwa ajili ya viwanda vya bia vilivyopo chini ya kampuni ya TBL na kukutana na Vitus Mhusi huwezi kujua kuwa ni Meneja Mkuu wa kiwanda kutokana na muda wote anavyokuwa anachapa kazi  na kusimamia shughuli za uzalishaji kwa karibu kuhakikisha zinaenda vizuri.

Kwa kuzingatia misingi  ya uongozi bora Vitus muda wote huwa na ukaribu na wafanyakazi wenzake na lijitokezapo tatizo la kikazi kama vile mitamo kuwa na hitilafu huakikisha analivalia njuga kwa kushirikiana na wafanyakazi waliopo chini yake kulitatua nafasi aliyonayo  sio ya kubahatisha bali anao ujuzi na uzoefu wa muda mrefu akiwa amefanya kazi katika viwanda vya bia vya TBL nchini kwa zaidi ya miaka 35.

Katika mahojiano hivi karibuni Vitus alieleza kuwa akiwa msomi wa fani ya sayansi upande wa kemia ametumia elimu yake katika maisha yake  yote kufanya kazi inayohusiana na uzalishaji wa bia .

“Najivunia na kazi yangu na naipenda kwa kuwa utaalamu wangu unachangia kuzalisha vinywaji vya bia bora ambazo zinatumiwa na watu wengi sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi”.Alisema na kuongeza kuwa awaonapo wanywaji wakiburudika na kinywaji cha bia husikia furaha sana na hasa ikizingatiwa kuwa wapo watumiaji wengi ambao wanatumia kinywaji cha bia bila kujua kuwa wataalamu wa kukitengenezwa wanatokea kwenye jamii wanazoishi na ni watu wa kawaida.

Akielezea historia ya maisha yake Vitus ambaye katika maisha yake yote amefanya kazi katika kampuni ya TBL anasema kuwa ni msomi mwenye shahada ya Sayansi ya Kemia na Takwimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwaka 1987.

Alisema baada ya kuhitimu aliajiriwa na kampuni ya TBL kama mtaalamu wa maabara kazi ambayo aliendelea nayo hadi alipofanikiwa kupata nafasi ya kuongeza ujuzi katika fani ya kutengeneza bia katika Chuo Kikuu cha Heriot Watt nchini Scotland kwa kipindi cha mwaka mmoja kati ya mwaka 1992 hadi mwaka 1993.

Kabla ya kushika wadhifa alionao hivi sasa amepitia ngazi mbalimbali za uongozi wa vitengo kwenye viwanda vya TBL “.Nimeongoza vitengo mbalimbali katika kampuni ya TBL na nimejifunza mambo mengi yanayohusiana na misingi ya utawala bora na uzalishaji wenye viwango”.Alisema.

Aliongeza kuwa kufanya kazi kwake sehemu mmoja katika maisha yake kumemuwezesha kuielewa vizuri sekta ya uzalishaji bia kwa undani pia ameweza kuhudhuria kozi nyingi za ndani zinazotolewa kwa wafanyakazi  na  aliifananisha TBL Group  na Chuo cha mafunzo kutokana na kuwa na mafunzo ya aina mbalimbali na ya kila mara kwa wafanyakazi wake ambayo yanawasaidia wakiwa kazini na nje ya kazi.

Kuhusiana na mafanikio aliyoyapata kwa kufanya kazi katika  kampuni ya bia, alisema ni mengi ikizingatiwa kuwa anafanya kazi kwenye kampuni kubwa inayojali maslahi ya wafanyakazi wake “Mafanikio ni mengi ndio maana sijahama kwenda sehemu nyingine tangu nianze kazi zaidi ya miaka 35 iliyopita,kutokana na kazi hii naweza kuihudumia vizuri familia yangu”.Alisema.

Maoni yake kuhusiana na kukua kwa sekta ya uzalishaji vinywaji nchini alisema hivi sasa imekua  tofauti na miaka ya nyuma ambapo hapakuwepo na ushindani katika sekta hii kama hali ilivyo kwa sasa.

Kuhusiana na changamoto anazokutana nazo kwenye kazi yake alisema kuwa ni za kawaida kwa kuwa hakuna kazi yoyote ambayo haina changamoto kinachotakiwa ni kukabiliana nazo na kusonga mbele.

Mbali na kazi za kiwanda Vitus alisema kuwa ni mpezi wa michezo mbalimbali hasa mchezo wa soka ambapo miaka ya nyuma alipokuwa kijana alikuwa mchezaji wa kutumainiwa wa timu ya soka ya Pilsner iliyokuwa chini ya kampuni ya TBL ambapo hivi sasa baada ya kuacha kucheza soka amekuwa akishiriki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon ambayo yamekuwa yakiandaliwa na kampuni anayofanyia kazi ya TBL Group na kufanyika mkoan Kilimanjaro kila mwaka na kuwavutia washiriki kutoka nchi mbalimbali.

Kuhusu maisha yake ya baadaye baada ya kustaafu alisema kuwa atajihusisha na shughuli za kilimo na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na fani yake.


Alimalizia wa kutoa wito kwa vijana waliopo mashuleni kusoma kwa bidi li kupata taaluma zitakazowawezesha kufanya kazi kitaalamu na  kuleta mabadiliko a kwa vijana waaoairiwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na kiu ya kujiendeleza bila kusahau uwa wavumilivu na waaminifu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)