Pages

HILARY CLINTON "APIGWA", TAJIRI DONALD TRUMP ASHINDA KURA ZA MCHUJO


NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya Habari
HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti charais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.
Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne usiku.
Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.
Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo Clinton ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)