Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.
Na Mwandishi Wetu, Arusha.
NaibuWaziriwaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe.
Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha,
ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo.
Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha,
ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo.
Naibu Waziri huyo pia amewahimiza watendaji wa MSD kuwa waadilifu, kuwajali na kuwasilikiza wateja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja, huku akitoaangalizo kwa wale wanao kiuka taratibuza ajira kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhaminiya MSD Prof. IdrisMtulia ameeleza kuwa MSD inaweza kufanya vizuri zaidi endapo changamoto za sheria ya manunuzi, mgawo mdogo wafedha kwa vituo vya Afya, hospitali na zahanati, na mgawo wafedha kuja kwa mafungu zitafanyiwa kazi.
Naye Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa MSD itakuwa na maduka manne tu mkoani Dares Salaam, Mwanza, A Arusha na Mbeya ambapo kwa mikoa mingine MSD wanaafanyama wasiliano na hospitali za mikoa ziwe na maduka ya hospitali wanayoendesha wenyewe na kisha MSD iwauzia dawa na kuwawezesha utaalamu wakuendesha maduka hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)