Pages

BASI LA BM LAPATA AJALI WATU WAWILI WAFARIKI NA WENGINE 43 WAMEJERUHIWA

          Basi la BM baada ya kupata ajali. 
Abiria 2 wamefariki dunia na wengine 43 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi la BM lenye namba za usajili T 619 BQX lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kwenda Morogorogo kupinduka jana usiku. 
Mashuhuda wamesema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika eneo la Lubungo - Mikese katika barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam jana saa tatu na nusu usiku. 
Chanzo cha ajali hiyo inaelezewa kuwa ni mwendo kasi wa dereva la basi hilo, ambapo aligonga lori lililokuwa linakuja mbele yake hivyo kusababisha basi hilo kupinduka zaidi ya mara mbili upande wa pili wa barabara ambako kuna bonde. Majeruhi walikimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)