Mwanamuziki Ali Kiba na Victoria Kimani wakiwa katika onyesho la Coke Studio
Wanafunzi kuanzia shule za msingi nchini hadi vyuo vikuu wameshiriki kuonyesha vipaji vyao katika msimu huu wa Coke Studio kama wanavyoonekana katika moja ya tamasha la Coke Studio
Mwanamuziki Fid Q akitoa burudani katika moja ya tamasha la Coke Studio
Wasanii wa muziki wakitoa burudani katika moja ya tamasha la Coke Studio mkoani Mwanza
Wanafunzi na vijana
mitaani waendelea kupata burudani
Onyesho la Coke Studio msimu wa tatu linaloendelea linazidi
kuleta burudani na furaha kwenye makundi mbalimbali ya jamii na kuacha gumzo
kwa wengi nchini.
Vijana wengi wameeleza kuwa pamoja na kuburudika na maonyesho ya kolabo za wanamuziki machachari
yanayoonyeshwa kupitia luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi na kwenye redio
ya Clouds bado wamekuwa wakipata burudani kutoka matamasha shirikishi
yanayoendelea kwenye mikoa mbalimbali na kushirikisha watu kutoka makundi
mbalimbali ya jamii.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walipohojiwa juu ya onyesho
hili walisema kuwa linaleta raha na burudani huku likiibua vipaji na
kuwakutanisha vijana na watu wanaojiamini ambao wamefanikiwa kwenye mambo
wanayoyafanya.
“Coke Studio ni zaidi ya burudani kwa kuwa pia inatuwezesha
vijana kuonyesha vipaji wakati huo huo kukutana na watu ambao wanajiamini ambao
wamefanikiwa katika mambo yao ”.Alisema
Willy Chale Mwanafunzi wa Sekondari ya Mwanza.
Miriam Chande mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa fedha alisema
analipenda onyesho la Coke Studio kwa kuwa linatoa burudani ya aina yake ya
muziki ambayo imewalenga vijana na inawawezesha kupata jumbe za kuwahamasisha
kusonga mbele kimaendeleo.
Kassim Juma,mwendesha bodaboda na mwanamuziki wa kujitegemea
amesema kuwa yeye na wenzake wanapenda onyesho la Coke Studio kwa kuwa ni la
viwango na limelenga kutoka burudani kwa
makundi mbalimbali kupitia kuangalia kolabo za wanamuziki na matamasha
ya muziki na burudani yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini.
Msimu wa Coke Studio mwaka huu umeshirikisha wanamuziki
mbalimbali kutoka Tanzania
na nchi za nje
Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up) na
Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki
2face kutoka Nigeria , Ali Kiba na
Victoria Kimani na Ben Paul na wangechi.
Msimu huu wa Coke Studio umeambatana na kampeni mpya yenye jina
la ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, na hivyo kujumuisha vijana mbalimbali ambao
wanaamini katika kufikia malengo yao bila ya kujali changamoto zinazowakabili.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja
wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti
hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto
ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)