MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAFANYIKA SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YAFANYIKA SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Soko la Temeke Sterio Amani Mtemi akiwatambulisha wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Temeke, John Bwana.
 Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe akisoma risala ya Shirika hilo kwa mgeni rasmi.
 Mdau Mwajuma Issa akichangia jambo kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia hasa matusi wanayofanyiwa na wanaume katika soko hilo.
 Kijana Andrew Kamtu akielezea chanzo cha ukatili wa kijinsia kuwa kinaanzia kwa wazazi wenyewe.
 Ofisa wa EfG, Charles akigawa vitabu vya msaada wa kisherea kuhusu ukatili wa kijinsia.
 Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia kutoka Mkoa wa Kipolisi Temeke wakiwa kwenye maadhimisho  hayo.
 Wakina mama wakiserebuka kwenye maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea.


 Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wawezeshaji sheria masokoni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Burudani zikiendelea kutoka kwa kundi la Machozi Theatre Group.
 Wananchi wakifutilia maadhimisho hayo.
 Ngoma ya mganda ikichezwa ikiongozwa na chipukizi kutoka kundi la Machozi Theatre Group.
 Burudani ya Sarakasi hiyo ikifanyika.
 Hapa ni furaha tupu.
 Mwezeshaji Sheria  Kashindye Kapambala akichangia jambo kuhusu ukatili wa jinsia.
 Wanawake wakitembea katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Machozi Theatre Group wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa sheria masokoni akichangia jambo kuhusu ukati wa kijinsia masokoni unavyofanyika.

Na Dotto Mwaibale

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha  jamii kuhusu kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo kusaidia kupunguza vitendo hivyo nchini.

Hayo yalibainishwa na Ofisa wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Meshack Mpwaga katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika Soko la Temeke Dar es Salaam leo mchana yaliyokuwa na kauli mbiu " Funguka chukua hatua mlinde mtoto apate elimu"

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo yaliyoa andaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG), Mpwaga alisema mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kiasi kikubwa yameisaidia nchi katika kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ambapo uelewa umekuwa mkubwa.

"Uelewa kwa jamii kuhusu vitendo hivyo ni mkubwa mno wito wangu jamii iendelee kutoa taarifa polisi pale inapobaini kuwepo kwa vitendo hivyo nasi tutachukua hatua stahiki" alisema Mpwaga.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Temeke, John Bwana,  ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ametoa mwito kuwa siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia jamii izitumie kuelimishana  na kupambana na ukatili huo wa kijinsia.

Alisema ni muhimu sasa jamii kuelimika na kuachana na vitendo vya udhalilishaji sehemu yoyote ili kupata taifa la watu waliostaraabika.

Alisema serikali hasa idara ya maendeleo ya jamii imekuwa ikisaidia na taasisi binafsi katika kupiga vita vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia jambo linalosaidia jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa uhuru.

Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG, Grace Mathe alisema utafiti uliofanywa na shirika juu ya ukatili dhidi ya wanawake masokoni unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta isiyo rasmi wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na matusi katika maeneo yao ya kazi.

Alisema mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Temeke na Ilala ndani ya masoko sita ambayo ni Feri, Kisutu, Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na Temeke Sterio na kuwa umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo rasmi hususani wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages