Party ya uzinduzi wa filamu ya James Bond, Spectre ilivyofana - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Party ya uzinduzi wa filamu ya James Bond, Spectre ilivyofana

Mwigizaji  WemaSepetu  (kushoto) akifurahia jambo na mwakilishi wa  kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  
Mulamula, wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James  
Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.
Bond Girls posing at the Jaguar 2
Wadau wa Belvedere Vodka pamoja na Heineken wakishow some love
Mchekeshaji ambae pia ni mshereheshaji Evance Bukuku akizungumza na Tanya Mulamula ambae ni mwakilishi wa  kampuni ya QWAY chini inayosambaza kinywaji cha 

Belvedere Vodca pamoja na Moët-Hennessy  wakati wa hafla ya uzinduzi wa
filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market

Mwakilishi wa kampuni ya QWAY International inayosambaza kinywaji  cha Belvedere Vodka nchini, Tanya  Mulamula, kulia akiwa na Carlo wa Nyama Choma Festival  wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market.
Bond Girls posing at the Belvedere Bar
Bond Girls posing at the Heineken DJ Booth

Na Mwandishi Wetu

WATU 
mbalimbali walihudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Spectre ya 
James Bond iliyofanyika Cape Town Fish Market chini ya udhamini wa 
Belvedere Vodka, Heineken, Jaguar pamoja na Land Rover.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, mwakilishi wa kampuni ya  QWAY International inayosambaza  kinywaji cha Belvedere Vodka,Tanya Mulamula alisema hafla hiyo inalenga kuwakutanisha wadau na kuifurahia  filamu hiyo, ikiwa siku moja kabla ya uzinduzi wake.



Filamu ya  hiyo ya Spectre iliyoigizwa na Daniel Craig kama James Bond ilizinduliwa rasmi hapa nchini Ijumaa iliyopita uzinduzi uliofana.

 
Alisema kuwa  kinywaji hicho kinatambua nafasi ya filamu katika kuwaburudisha wateja  wake na ndio maana imetoa tiketi nyingi za bure kwa wateja wake wengi.

 
Belvedere Vodka, Heineken, Land Rover na Jaguar tumeamua kwa pamoja 
kuungana na watu wengine wengi katika kusherehekea uzinduzi wa filamu 
hii kwa kuanza na hafla hii ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa 
filamu yenyewe" alisema Tanya.

 
Pia Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya  
CMC inayohusika na magari ya Jaguar pamoja na Land Rover, Kim Withnall  
alisema kuwa filamu hiyo imehusisha magari ya Jaguar na Land Rovers na  
ndio maana hata kwa Tanzania kampuni yake imeshiriki katika kuandaa  
hafla hiyo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages