
Miaka 10 iliyopita secta ya ajira ilikuwa tofauti
sana na ilivyo leo hii, utaftaji wa ajira ulikuwa ni tofauti sana na ilivyo
hivi sasa. Matangazo ya ajira yalikuwa yakitegemea zaidi magazeti na serikali
kufikia hatua ya kufanya ni lazima kila kampuni binafsi na hata mashirika ya uma
kutangaza ajira mpya kupitia kwenye kurasa za magazeti.
Wengi wetu tuna fahamu kuwa magazeti kama vile
Daily News, Mwananchi, The Guardian pamoja na The citizen ndiyo magazeti maarufu
sana katika kutangaza matangazo ya ajira.
Magazeti haya ambayo huchapishwa kila siku
yamekuwa msaada mkubwa sana kwa wale wanao tafuta ajira na sehemu kuu ya kusoma
ajira mpya zinazotangazwa kila kukicha basi ni kwenye kurasa za magazeti haya.
Mabadiliko ya tekinologia yamekuja kimageuzi
kwenye secta hii na kuongeza urahisi zaidi kwa watafutaji wa ajira hapa nchini
Tanzania. Kuanzia mwaka 2007 ndipo mabadiliko haya yalipo anza kuibuka baada ya
tovuti mbali mbali zinazotoa matangazo ya jira mitandaoni kuibuka kwa kasi
zaidi.
Ukuaji huu wa mitandao ya matangazo ya ajira
imeleta mabadiliko ambayo leo hii imekuwa ni faida sana kwa pande zote mbili
mbazo ni watafuta wa ajira na waajiri.
Asilimia 80 ya makampuni yanayo jishughulisha na
kutafutia waajiri wafanya kazi, wengi wetu tukiyafahamu kwa lugha ya kigeni
“Recruitment Agencies” wana weka matangazo yao kwenye mitandao.
Tovuti kama vile Jobstanzania
nao pia wameongeza wigo na kurahisisha zaidi huduma hii kwa kuanzisha tovuti
inayo toa taarifa za matangazo ya ajira kila siku. Ambapo pia wana toa fursa
kwa waajiri kuweka matangazo ya ajira kwenye mtandao bure kabisa.
Achilia mbali urahisi huu wa kupatikana kwa
matangazo ya ajira, hivi sasa tekinologia pia imerahisisha hata pia njia za
uombaji kwa wanao tafuta ajira. Hapo awali njia kuu yakutuma maombi ya ajira
ilikuwa ni kupitia posta lakini leo hii kuna mabadiliko makubwa sana ikiwa
waombaji wa ajira wanaweza kutuma maombi kwa barua pepe (Email) na kumfikia
mwajiri kwa haraka zaidi.
Japokuwa tatizo la ajira kwa vijana wanao hitimu
chuo kwa sasa limezidi kuwa kubwa, hii ni kiashirio kuwa sasa vijana
wanajiendeleza kielimu lakini tatizo ni ajira. Serikali inajitahidi sana
kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira lakini bado kuna uhaba wa ajira.
Suluhisho ni nini?
Unaweza jiuliza je ni vijana wangapi wana hitimu
kwenye vyuo vikuu vyetu hapa Tanzania? Jibu ni maelfu na hawa wote wanahitaji
ajira wakati huo huo ajira bado ni chache sana.
Nini Kifanyike?
Ajira sio suluhisho, kuna fursa nyingi sana kwa
vijana kufanya na kujikwamua kiajira kwa kujiajiri wenyewe. Naamini katika vyuo
vyetu vina fundisha somo la ujasiliamali (Entrepreneurship), basi kama vijana
wanao hitimu vyuo wakitilia maanani somo hili na kutafuta fursa za wao
kujiajiri naamini janga la ukosefu wa ajira litakuwa na kikomo.
Je! wewe una mtazamo gani? toa maoni yako kupitia
kwenye sehemu ya kutoa maoni hapa chini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)