#UchaguziTZ2015: Wakazi wa Segerea Wajitokeza kwa Wingi kupiga kura - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

#UchaguziTZ2015: Wakazi wa Segerea Wajitokeza kwa Wingi kupiga kura

 Wakazi wa Segerea ambao wamjiandikisha katika kituo cha Segerea Magereza wakiwa wamejitokeza kwa wingi muda huu katika kituo hiko kwaajili ya kushiriki zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia Rais, wabunge na Madiwani. Hali ni shwari hakuna vurugu wala viashiria vyovyote vile vya vurugu japokuwa kuna changamoto za hapa na pale ambapo mkazi mmoja ameambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kupiga kura kutokana na namba ya Kitambulisho chake cha kupigia Kura kutofautiana tarakimu moja tu na Namba ya kitambulisho iliyoandikwa katika karatasi la majina ya kuhakiki. Mkazi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa anasubiri Mkuu wa kituo cha Uchaguzi Segerea Magereza kuweza kuongea nae na Kutatua swala hilo endapo ataruhusiwa basi atapiga kura na asiporuhusiwa basi hatopiga kura
Wakazi wa Segerea wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura
Baadhi ya wakazi wa segerea wakiwa katika foleni tayari kwa kupiga kura.Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Endelea kuwa nasi hapa tutakuletea kila kinachojiri kwenye vituo vilivyo karibu yetu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages