
Picha kwa Hisani ya AP.
Leo ndio Siku iliyokuwa ikisubiriwa sana na watanzania kwaajili ya kuchagua viongozi wa Tanzania kwa awamu ya tano , Baada ya safari ya miezi miwili na Siku mbili za Kampeni kumalizika hapo jana katika mikoa tofauti Hatimaye Leo Wananchi wana kazi moja tu ya Kuchagua viongozi wanaowaona wanawafaha au watakaowaletea Maendeleo , uchaguzi wa Mwaka 2015 ni uchaguzi wa historia katika taifa hili kutokana na Kutokea kwa Hamasa kubwa kwa wakazi wake huku kikubwa cha Kufurahisha ni kwamba Hata wale wapinzani ambao ni mashabiki wa vyama tofauti wakiwa wamoja na kusema kuwa Kuna maisha baada ya uchaguzi hii inaonyesha kabisa kuwa Siasa sio uadui.
Hali hii ya upendo na amani baina ya wapinzani tuna amini itaendelea mpaka siku ya mwisho ambapo rais ataapishwa. Wito wetu Kwa watanzania tunawasihi wajitokeze kwa wingi kwenda kutumia haki yao ya msingi na kikatiba ya kuchagua viongozi wawatakao kuwaongoza kwa awamu ya tano.
Kikubwa ni kufuata sheria na taratibu za uchaguzi huku tukisubiri matokeo kutangazwa. Tunaamini uchaguzi utakuwa wa huru na haki
Lukaza Blog inawatakia Watanzania wote Uchaguzi Mwema huku tukitarajia utulivu na amani wa hali ya juu katika kipindi hiki cha Uchaguzi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)