WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI WAKISUBIRI JINA LA MGOMBEA URAIS KUPITIA UKAWA USIKU HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI WAKISUBIRI JINA LA MGOMBEA URAIS KUPITIA UKAWA USIKU HUU

Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari  hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum jijini Dar es Salaam,Makene amesema majadiliano hayo sio urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Makene amezidi kuwataka waandishi wawe na subira kusubiri maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo. 
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana,Waandishi wa Habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam,wakajikuta wanaacha stendi za Camera zao na kukaa pembeni kama zionekanavyo pichani usiku huu,wakisubiri lolote litakalojiri.
Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa leo ndio siku rasmi ya kutangaza jina hilo lakini masaa yanazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.
Waandishi wakisubiri mtu wa kutoa taarifa juu ya jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, ambapo taarifa hizo za kuja mtu huyo ziligonga mwamba na kuambiwa kilichobaki ni makubaliano suala jinsi kuendesha uchaguzi katika majimbo.
Waandishi wakijadiliana masuala yanayohusu tasinia ya habari baada muda mrefu kuletewa jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum ,Masaki jijini Dar es Salaam.

Waandishi wakiwa katika viyunga vya hoteli ya Colesseum wakisubiri jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA
Waandishi wakiwa wamechoka na uchovu wa kusubiri jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colesseum leo jijini Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya Jiachie Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages