MHE.EDWARD LOWASSA AKARIBISHWA RASMI KUJIUNGA NA UKAWA.,MGOMBEA URAIS KUTANGAZWA AGOSTI 4 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MHE.EDWARD LOWASSA AKARIBISHWA RASMI KUJIUNGA NA UKAWA.,MGOMBEA URAIS KUTANGAZWA AGOSTI 4

 Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar
  Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
 Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar.
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana  kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)
  Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
   Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya kuzungumza na Waaandishi wa Habari  makao makuu ya chama cha CUF,mapema leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
UMOJA wa  katiba ya Wananchi  nchini (UKAWA) vinamkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika  na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika kuweza kusimamia nchi.

Mbatia amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu  Mstaafu,Edward Lowassa kutokana na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na uwezo anao katika kusimamia.Amesema  akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana na kutambua kuwa ni mhamasishaji  na  ni mtu mwenye kuthubutu.

Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea  mmoja katika kila nafasi kupeperusha bendera  ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka  huu.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba
amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo  uliopo. 
Amesema  wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka  huu  na atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.

Mbatia hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma
wamefikishwa mahakamani .

Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na  tuhuma zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa  umeme wa dharula kupitia kampuni ya Richmond.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages