Kuchagua
rangi rafiki kwa mazingira wakati wa upambaji hakufanyi tu hewa ya ndani kuwa
safi lakini pia hutunza mazingira. Hewa safi na nzuri ni jambo la kwanza kwa
nyumba inayozingatia mazingira. Kwa Bahati mbaya, kuna matatizo makubwa sana ya
kiafya yanayoletwa na sumu zinazowekwa katika rangi kwa lengo la kuongeza ubora
wa rangi hizo. Sumu hizi ni pamoja na risasi, zebaki, aseniki na Kromiam.
Utafiti wa
mwaka 2002 uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Marekani ulibaini kuwa wanawake
na wanaume wanaofanya biashara ya rangi wamekuwa katika hatari kubwa ya kupata
saratani, matokeo yanayoonesha rangi zenye sumu zinaweza kuwa za hatari kwa
afya zetu na mazingira.
Shirika la
afya duniani linasema kuwa wataalamu wa upambaji wana asilimia 40 ya hatari
kupata kansa ya mapafu. Wanasayansi kadhaa wamethibitisha kuwa vitu vya hatari
kama aseniki, risasi na zebaki husababisha kutokea kwa magonjwa ya mishipa ya
moyo. Aseniki pia inapelekea kulainisha mifupa, saratani zinazosababishwa na kromium
na magonjwa ya kurithi, zebaki huweka sumu kwenye mfumo wa fahamu na figo na
risasi husababisha matatizo ya saratani.
Kuanzia miaka
ya 2010, wazalishaji rangi walilazimika kukubaliana na masharti ya kupunguza
viwango vya sumu vinavyotumika katika rangi ili kuongeza ubora wake ikibidi
hata kutotumia kabisa. Kampuni ya Insignia Limited, gwiji wa uzalishaji rangi
nchini Tanzania imekuwa mzalishaji rangi wa kwanza kabisa kutoa rangi rafiki wa
mazingira. Tangu mwaka 2012 kiwanda kimechukua hatua muhimu Kuanzisha utoaji wa
rangi rafiki kwa mazingira. Bidhaa zote za upambaji zinazozalishwa na kiwanda hicho
hazina nyongeza ya risasi, zebaki, aseniki na kromiamu ambazo zimethibitishwa
kuwa na madhara makubwa kwa afya na mazingira.
Kwa mujibu wa
Bw Kishan Debar Mkurugenzi mtendaji wa Insignia Limited (Coral Paints), Hatua hii
ya kipekee iliyochukuliwa na kampuni inasukumwa kwa utambuzi wa wajibu wa
kutunza mazingira na afya za Watanzania. Marekebisho yaliyofanyika katika rangi
hayaathiri ubora wa rangi na bajeti ya mtumiaji.
“Ni kazi na wajibu wa kila mmoja kulinda
mazingira wanayoishi na wanapofanyia kazi. Biashara yetu ni kufanya makazi na
vitu kuwa vizuri na vya kudumu. Tunawezaje kuyasahau mazingira ambamo nyumba
zetu zimejengwa. Tunafanya kila tuwezalo kusaidia kulinda mazingira tunayoishi
kwa kuwa ni kitu tunachokithamini na kinachotuwezesha kuishi”. Alisema Bw
Kishan akichangia.
“Haina maana kuwa ili kutengeneza rangi
zinazoendana na mazingira tunaondoa ubora wake. Rangi tunazozalisha zinaenda na
viwango vya kimataifa na kwa gharama nafuu, zinafanya kazi kwa kiwango cha juu,
ni suluhisho lenye ubora na la kudumu lisilo na madhara” . “Coral paint inatoa
rangi rafiki kwa mazingira pasipo kuongeza gharama zozote kwa mtumiaji”. Anasema
Bw Kishan aliyeishukuru timu yake ya utafiti na maendeleo ndani ya Insignia
Ltd.
Kuhusu Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia
kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya
rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa
sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.
Hivi leo, Insignia imefikia moja
ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika
utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango
vya hali ya juu nchini Tanzania
umewezeshwa na ushirikiano na makampuni
makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal
iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco
ya Ufaransa.
Bidhaa mbili za Coral na Galaxy,
zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni
inatengeneza rangi na bidhaa nyingine
nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia
kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatengenezwa
kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake
teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika
soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye
ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.
Kiufanisi, miundombinu ya Insignia
inajulikana kwa ubora wake. Viwanda vyake
vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya
kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini
Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi,
Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana
wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa
nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)