Ikisherehekewa
kila mwaka tarehe 14 Juni Siku ya kimataifa ya uchangiaji damu inahusika katika
kuinua uelewa wa umuhimu wa kila mmoja kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha na pia
kutoa shukrani kwa wachangiaji damu wote duniani. Katika nchi zinazo kua kama
Tanzania upatikanaji wa damu salama ni bidhaa adimu na hasa inachangiwa na
ushiriki mdogo wa raia.
Hata
hivyo pamoja na shughuli zote zinazofanyika katika siku hiyo ni muhimu sana
kila mmoja kutambua umuhimu wa kuchangia damu kwa hiyari. Hospitali inayoongoza
kimataifa ya Apollo ni moja kati ya taasisi zilizotumia fursa hii kutoa wito
kwa watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangiaji damu sababu ya umuhimu wake
katika matibabu. Mwanzilishi na
mwenyekiti wa hospitali za Apollo Dkt Prathap C Reddy anasema “kutoa damu ni rahisi na kunaokoa maisha,
upatikanaji wa mfumo wa kuongezewa damu nchini unatoa nafasi ya uhai kwa watu
bila kujali jinsia au umri”.
Kwa
wastani inakadiriwa kuwa duniani kote damu milioni 92 zinatolewa ingawa
upatikanaji wa damu salama unahitajika zaidi hasa kwenye nchi kama Tanzania. Kwa
mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa shirika la taifa la uchangiaji damu
(NBTS) mahitaji ya damu salama Tanzania ni karibu chupa 400,000 hadi 450,000 za
mililita 450. uchache wa wachangiaji unamaanisha kuwa mahitaji kitaifa
hayajafikiwa, katika robo ya mwaka 2015 pekee chupa 18,000 zilikusanywa. Katika
nchi ambayo taasisi kubwa za afya kama Muhimbili zinahitaji chupa zaidi ya 50
kila siku namba hiyo inaonesha hatari kubwa sana.
Kwa kuwa kuchangia
damu ni tendo la hiyari Dkt Reddy anatoa
wito kwa raia kuona umuhimu ambao tabia ya uchangiaji damu inaleta kwa wananchi
wenzao. Tofauti na madawa na vifaa vingine vya matibabu damu haiwezi kuzalishwa
kiwandani na chanzo pekee ni uchangiaji. Mtu anayefanikiwa kuishi maisha marefu
kiasi kuna wakati katika maisha yake atahitaji damu au bidhaa za kuongeza damu
lakini cha kushangaza ni kuwa asilimia tano tu ya watu huchangia damu mara kwa
mara.
Dkt. Reddy wa hospitali za Apollo anaendelea kueleza
kuwa “watu wengi hawashiriki kitendo hiki
cha ukarimu hasa kwa sababu ya taarifa potofu ikiwemo kutokuelewa hatua za
uchangiaji”, Sababu kubwa hasa ikiwa uoga wa kupata maambukizi wakati wa
mchakato wa utoaji damu. Utimiaji wa mifuko inayoteketezwa kwa kuhifadhia damu
na sindano salama kabisa unahakikisha kuwa watu hawawezi kupata maradhi ya
kuambukiza kama VVU katika mchakato wa uchangiaji damu. kufuatia uchunguzi wa
kimaabara uliofanyika kuangalia dalili za Hepatitis (B&C), Malaria,
VVU/Ukimwi, magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na kutambua makundi ya damu ndipo
damu inatumika kwenye matibabu.
Damu iliyotolewa
ina matumizi mengi katika matibabu, baada ya utoaji na hatua za uchunguzi damu
inatengwa katika vipengele vyake tofauti tofauti. Seli nyekundu za damu
zinatumika kuongezea damu iliyopotea kwa majeruhi na wagonjwa waliofanyiwa
upasuaji. Plazma mbichi iliyoganda ambayo ni sehemu ya majimaji ya damu
inatumika hasa kwa wagonjwa wenye matatizo ya Ini, majeraha ya kuungua na na
kesi za aina hiyo. Chembe za kugandisha damu ambazo husababisha kuganda kwa
damu wakati mtu anapojikata au anapopata jeraha la wazi, hii huwa inatumika kwa
wagonjwa wa lukemia na upandikizaji viungo.
Uchangiaji damu wa
hiyari ni wa muhimu sana katika matibabu, ni kitendo kisicho cha kichoyo na
upekee wake ni kuwa ni mchangiaji anayeunda mhimili wa benki za damu na hivyo kuweka msingi salama na wa kuaminika
katika mfumo wa uongezewaji damu nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)