Mfumo wa upasuaji wa kiroboti usiotumia
kisu (Cyberknife) ni njia m’badala ya upasuaji usiokuwa na madhara kwa matibabu
ya uvimbe wa saratani na usio wa saratani popote katika mwili, hii ni pamoja na
kibofu, mapafu, ubongo, uti wa mgongo, ini, kongosho na figo. Matibabu
yanayotoa mihimili ya kiwango cha juu ya mionzi kwa uvimbe uliokomaa- yanatoa
matumaini mapya kwa wagonjwa duniani kote.
Mfumo wa upasuaji wa kiroboti
unaotumia mionzi unaboresha mbinu nyingine za upasuaji kwa mionzi kwa kuondoa
mahitaji ya baadhi ya vifaa vya upasuaji. Matokeo yake, upasuaji usiotumia kisu
unawawezesha madaktari kufanikisha kiwango kikubwa cha usahihi pasipo kuwa na
madhara na inaruhusu wagonjwa kutibiwa bila kulazwa. Mfumo huu usiotumia kisu
unaweza kuonesha eneo sahihi ulipo uvimbe kwa kutumia picha za mionzi (X-ray)
zinazokuwa zimechukuliwa wakati wa kutibu saratani zinazoonesha utofauti wa
muundo wa mifupa ya kichwa cha mgonjwa.
Mfumo huu una rekodi imara ya
ufanisi wa kliniki uliothibitika
(Cyberknife) Tiba isiyotumia
upasuaji katika kutibu saratani ya ubongo inahusisha timu, ambayo wataalamu
kadhaa wanashiriki.
Timu hii inaweza kuhusisha:
·
Mtaalamu wa upasuaji wa mfumo wa fahamu
·
Mtaalamu wa tiba ya mionzi
·
Mtaalamu wa madawa
·
Mtaalamu wa mionzi
·
Na madaktari wengine wasaidizi
Wakati wa hatua za awali za kupanga
namna ya kutibu pasipo kutumia kisu, taarifa za ‘CT, MRI na PET scan’
zitachukuliwa kwenye mfumo wa mpango matibabu Maalum (Cyberknife Systems treatment).
Timu ya madaktari itategemea ukubwa wa eneo muhimu litakalolengwa na mionzi na
kiwango cha mionzi. Pia watatambua eneo ambalo mionzi itatakiwa kupunguzwa. Kwa
kutumia taarifa hii, mfumo huu usiotumia kisu (Cyberknife) unatoa hesabu ya
mionzi inayohitajika kutibu uvimbe husika. Mpango matibabu huu unanufaisha
kikamilifu mfumo wa matibabu pasipo upasuaji kutumia kisu, inaruhusu matibabu
salama na sahihi zaidi
Matibabu ya uvimbe katika ubongo
hasa yanakamilika ndani ya siku 5. Kwa wagonjwa wengi, matibabu yasiyotumia
upasuaji kwa kisu (Cyberknife) hauna maumivu kabisa.
Wakati wa matibabu, mgonjwa analala
juu ya meza wakati uso wake ukiwa umekingwa kwa maski maalum. Mfumo huu wa
kompyuta unaoongozwa kwa roboti utazunguka mwili wa mgonjwa katika maeneo tofauti
tofauti ambako utafikisha mionzi kwenye uvimbe. Mgonjwa hatatakiwa kufanya
chochote isipokuwa kutulia akiwa amelala kwa kunyooka ipasavyo
Tiba hii inapokamilika tu, wagonjwa
wengi hurudi kwenye ratiba zao za kila siku haraka pasipo kuvuruga shughuli
zao.
Baada ya kumaliza tiba ya mionzi,
ni muhimu kwa mgonjwa kufwata ratiba na kuhudhuria kama atakavyoambiwa na
mtaalamu. Ni muhimu pia kuelewa kuwa uvimbe hautapotea haraka. Kupona
kunatofautiana kati ya mgonjwa na mgonjwa Uzoefu umeonesha wagonjwa wengi
wanapokea vizuri tiba ya hii isiyohitaji upasuaji kutumia kisu. Kwa kufwatilia,
madaktari wataangalia matokeo kwa miezi na miaka ya matibabu ya mgonjwa, mara
nyingi kwa kutumia ama ‘CT scan’ na/au
‘PET-CT scans’.
Imechangiwa na:
Dkt RATHNA
DEVI
MSHAURI
MWANDAMIZI TIBA YA MIONZI
IDARA YA
HUDUMA YA TIBA MIONZI NA,
MTAALAMU
WA SARATANI KATIKA HOSPITALI YA APOLLO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)