Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha mtu kujitegemea.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini.
Alisema kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa kwa sasa kutokana na vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto zinazokabili sekta hiyo pamoja na kuimarika kwake.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa uandikishaji wa watoto na mdondoko.
Alisema viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau wajibu wao na kumwachia mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na hii ndio chanzo kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya.
Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka wanakwenda wapi na wanafanya nini.
“kuna sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu hawachukia sheria hiyo” alisema.
Aidha alisema ubora wa elimu una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa walimu katika ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye maana.
Alisema kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu na usimamizi unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi unafanyika na mdondoko kuangaliwa.
Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa viongozi na wadau kutimiza wajibu wao.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya miaka miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma ya elimu.
Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima uangaliwe.
Aidha alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi ya elimu.
Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na wadau wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa lengo la kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na ubora wa elimu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) “Education For All 2000-2015” ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)