Mapema
wiki hii dunia iliungana kuadhimisha Siku ya Afya Duniani, kimataifa ni siku ambayo
huadhimishwa tarehe 7 Aprili kila mwaka. Siku hii imekuwa ikienda sambamba na masuala
ya kiafya na mambo mengine mbalimbali yanayotambua hatua zinazochukuliwa na
sekta ya afya katika kupambana na magonjwa. Katika miaka ya hivi karibuni
mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakifanya mabadiliko makubwa katika mfumo
wa huduma ya afya ili kuendana na viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Ulaya
na Marekani.
Mabadiliko
hayo yamesababisha uhitaji mkubwa wa huduma bora hasa kwa watu binafsi kutoka nchi
ambazo hazina uzoefu au azijapata mabadiliko. Katika maeneo mengi ya nchi hizo mabadiliko
haya na maendeleo ya kiafya yameunda sekta ya aina yake ijulikanayo kama utalii
wa kimatibabu (medical tourism)
ambapo watu kutoka mataifa mengine husafiri kwenda nchi maalum kwa sababu za
matibabu.
Mabadiliko
katika ubora wa huduma ya matibabu yamekuwa na matokeo makubwa katika sekta ya utalii
wa kimatibabu. Moja ya nchi zilizo mbele katika mabadiliko ni India, ambayo
inachangiwa na ukuaji mkubwa wa uchumi katika miaka ishirini iliyopita. India
inatambulika kama moja ya nchi inayopendelewa na watu duniani kwa matibabu ya
kina zaidi.
Kama
taifa linaloendelea gharama zinazotakiwa kwa ajili ya matibabu ni nafuu kulinganisha
na mataifa yaliyoendelea. Hii inawezeshwa na ukuaji wa miundombinu na vifaa
pamoja na teknolojia ya hali ya juu inayo ifanya India iwe sambamba na maendeleo
yaliyopo Marekani au Ulaya. Inakadiriwa kuwa mgonjwa kusafiri kwenda India kwa
sababu za matibabu unaweza kuokoa 70-75% ya jumla ya gharama bila kujali
anakwenda kwa ajili ya aina gani ya matibabu. Chama cha madaktari wa Marekani (American
Medical Association) hivi karibuni kilifanya utafiti juu ya gharama
zinazotakiwa kwa ajili ya upasuaji mbalimbali na matokeo kuonyesha kuwa India ina
gharama ndogo za matibabu, mara tatu chini ukilinganisha na nchi za magharibi
na bado ni kiasi kidogo ukilinganisha na mataifa mengine ya Asia. Kuchukua
mfano wa upasuaji wa goti katika maeneo mbalimbali, wastani wa gharama ni dola 40,000 katika hospitali za
Marekani, dola 10,000 katika hospitali za Thailand lakini India gharama ni dola 8,500. Kadhalika kwa
utaratibu kama vile kupandikizwa uboho nchini Uingereza gharama ni wastani wa dola
400,000, dola 150,000 Marekani ambapo India ni dola 30,000.
Tanzania
ni moja ya mataifa ambayo inafaidika kutokana na ukuaji wa sekta ya afya na
uchumi nchini India, ongezeko la wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya huduma za
matibabu kwa kiasi kikubwa linaonyesha watu wanapendelea kuchagua hospitali za
India. Ongezeko hili la watu halijachukua mkondo mmoja kwa kuwa taasisi
mbalimbali zimezingatia mwenendo huu na zimechukua hatua zaidi kuimarisha
uhusiano huu. Shughuli za mara kwa mara kama vile madaktari kutembelea Tanzania
kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali katika kutoa mafunzo kwa madaktari
Watanzania na kliniki za ushauri umejenga sifa ya taasisi ya afya ya India. Kwa
kufanya hivyo, imetoa uwezo wa kushinda moja ya vikwazo vikubwa vya utalii wa
kimatibabu ambavyo huwa ni vigumu kwa wagonjwa wengi kuweza kulipia gharama za msaada
zaidi wa matibabu pindi wanaporudi katika nchi zao.
Miongoni
mwa taasisi zinazofurahia uhusiano mzuri na Tanzania ni Hospitali za Apollo. Ikiwa
na majengo kadhaa nchini India, hospitali hio imekua na uhusiano mzuri na
wakuaminika kwa zaidi ya miaka 12 Tanzania. Kwa kuchochewa na gharama za chini na
uwepo wa vifaa, wengi wamechukua fursa hii kama njia ya kukwepa gharama kubwa
ya kwenda mahali pengine. Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuvutiwa na
hali nzuri ya huduma za afya zinazopatikana katika Hospitali za Apollo, mwaka
2003 kwa udhamini wa serekali kundi la watoto 20 waliohitaji upasuaji wa moyo
walipelekwa katika Hospitali ya Apollo Hyderabad. Vituo vya Apollo ziko katika
miji mikubwa kadhaa na zimekuwa zikivutia zaidi ya mataifa 150 mbalimbali ambazo
zaja kufanya ziara India kila siku. Vituo vya kisasa vya Apollo mjini Apollo Delhi,
Hyderabad, Chennai, Ahmedabad na Bengaluru ni miongoni ya zile ambazo zinafahamika
kwa kuvutia idadi kubwa ya wagonjwa wa nje.
Taasisi
ya Apollo inajivunia kuwa waanzilishi wa huduma bora na maendeleo yake
ikisababisha wapate tuzo mbalimbali. Miongoni mwa tuzo za juu ni ile ya Tume ya
Pamoja ya tuzo za kimataifa (the Joint Commission International
Accreditation (JCI))
ambayo ni kwa ajili ya hospitali zenye lengo la kuboresha ubora wa huduma ya
afya na usalama duniani kote. Katika hatua kipekee hospitali zake za mjini Delhi,
Chennai, Hyderabad, Ludhiana, Bengaluru, Kolkata, Mauritius na Dhaka zimefanikiwa
kupata tuzo hiyo. Na zaidi kituo chake cha Indraprastha Apollo Delhi kiliweka
historia kwa kuwa hospitali ya kwanza nchini India kwa kupata tuzo ya JCI mara
4 mfululizo. (i)
Kitovu
cha utalii wa kimatibabu ni Jiji la Chennai ambayo inajulikana kam mji mkuu wa
kimatibabu nchini India. Ni nyumbani kwa hospitali mbalimbali maalum na
inakadiriwa kuvutia wagonjwa 200 kila siku na 45% ya utalii wa kimatibabu
katika nchi hiyo. (ii)
Jiji la Chennai
linafurahia uhusiano mzuri na Afrika Mashariki, ina mkataba na Serikali ya Tanzania,
Kenya na Uganda ili kuhakikisha wananchi wanaohitaji tiba nje ya nchi wanapelekwa
Chennai kwa ufadhili wa serikali. Hili limekuwa na ufanisi katika kukuza sekta
ya utalii wa kitabibu Jijini hapo.
Wasiwasi
kuhusu ubora wa tiba katika nchi zinazoendelea kama vile India umekuwa ukijitokeza,
hata hivyo ni muhimu kutambua kwamba wataalamu wengi katika nchi hizi wamepata
mafunzo katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani na Uingereza, na hivyo
matokeo ya matibabu ni yanayolingana. Madaktari wenye sifa kitaaluma hufanya
kazi katika hospitali zilizotunukiwa tuzo mbalimbali si tu katika kutoa huduma za
kuaminika lakini pia kwa sukuma mipaka ya huduma za matibabu pamoja na kuja na
mbinu za kimapinduzi kufikia viwango vya kimataifa.
Taasisi
kama vile hospitali za Apollo hutumika kama ishara ya maendeleo, ikiwa imetokea
chanzo kidogo hadi kuwa moja ya watoaji wakubwa wa teknolojia ya juu ya afya pamoja
na vifaa bora na vya kisasa sambamba na nchi za Ulaya na Marekani. "Hospitali za Apollo ilifungua milango
yake mwaka 1983 na kuleta ubora wa kimataifa wa afya nchini India, kwa gharama
iliyoko chini mara kumi unapolinganisha na nchi za Magharibi. Hii ilikuwa mara
ya kwanza Apollo kuwajibika kijamii na sasa imekuwa moja ya watoaji wakubwa
duniani wa teknolojia ya huduma za afya katika viwango vya dunia ya tatu"
anasema mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dr. Prathap .C. Reddy.
Sekta ya
matibabu nchini India imetoka mbali katika miongo hii miwili hadi mitatu nyuma,
akitoa maoni juu ya mabadiliko haya Dr
Prathap c. Reddy alilinganisha sekta ya matibabu ya miaka ya nyuma India na
ile ya Tanzania leo na kusema kuwa "chati
ya Kujifunza kwa India inaweza kutumika kama jukwaa kwa ajili ya mataifa mengi
ikiwa ni pamoja na Tanzania kufikia hadi viwango vya kimataifa vya huduma za
afya” anasema kwamba "miundombinu
ya sasa na teknolojia inayotolewa katika maeneo kama Tanzania ni miaka 20 nyuma
ukilinganisha na dunia nzima" ikiwa ni wito kwa serikali na taasisi
binafsi kushinikiza mipaka ya huduma za matibabu kama wenzao kwa nia ya kuiweka
Tanzania kama nchi yenye ubora na yenye nguvu katika sekta ya afya ukanda wa
mashariki ya Afrika na zaidi.
Kuhusu hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo
ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa
kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa
karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika
elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".
Katika miaka 30 tokea
kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana
nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia
imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.
Katika safari yake, imeweza
kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120. Inatoa huduma
maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710. Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia
idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba. Imefanya
upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa
uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.
Taasisi ya Apollo ni moja
ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama
Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)