Siku ya figo Duniani inalenga kuongeza uelewa juu ya
umuhimu wa figo zetu, afya zetu kwa ujumla na kupunguza uwepo na matokeo ya
magonjwa ya figo na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo. Katika maadhimisho
ya siku hii Dkt. Kavita Parihar, mkuu wa “Nephrology” na idara ya upandikizaji
figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad anawatahadharisha Watanzania juu ya
dalili, hatari, matatizo, matibabu na uzuiaji kuhusiana na ugonjwa huu.
Ugonjwa sugu wa figo (CKD – Chronic Kidney Diseases),
ambao unajulikana pia kama kushindwa kwa figo, ni ugonjwa unayo athiri figo
hatua kwa hatua na kusababisha kushindwa kufanya kazi. Wakati ugonjwa sugu wa
figo unapofikia hatua ya juu, majimaji hatarishi, elektroliti na taka
zinajijenga katika mwili.
Katika Afrika, Magonjwa sugu ya figo huathiri watu wazima
hasa vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 50, na hasa ni kutokana na magonjwa ya
presha na “glomerular”, tofauti na nchi zilizoendelea, ambapo CKD inasumbua
zaidi wagonjwa wenye umri wa kati na wazee na utokana na ugonjwa wa kisukari na
shinikizo la damu. Dalili uchelewa kujionesha, 75% katika watu wanayo fikia hatua
za mwisho za magonjwa ya figo (ESRD) wanahitaji uchunguzi zaidi. CKD inatokea
mara 3-4 zaidi katika Afrika kuliko katika nchi zilizoendelea
Magonjwa
na hali ambayo mara nyingi inasababisha ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na:
- Kisukari
- Shinikizo la damu
- Magonjwa yanayoshambulia kinga ya
mwili (kama lupus, VVU na IgA neforopathy)
- Ugonjwa wa figo lenye uvimbe
- Kuziba muda mrefu kwa njia ya
mkojo, kutokana na hali kama vile kibofu kuwa kikubwa, mawe ya figo na
baadhi ya saratani
Mambo yanayoweza kuongeza hatari ya ugonjwa sugu wa
figo ni pamoja na:
- Ugonjwa wa kisukari, shinikizo la
damu, cholestrol kuwa juu na ugonjwa wa moyo
- Uvutaji sigara na uzito
kuzidi
- Kuwa na asili ya Afrika, Marekani
au Asia
- Historia ya ugonjwa wa figo kwa
familia
- Umri wa miaka 65 au zaidi
Dalili za ugonjwa wa figo:
- Kichefuchefu, kutapika na kupoteza
hamu ya kula
- Uchovu na udhaifu
- Matatizo ya usingizi, kupungua
uwezo wa akili na misuli kufyatuka / kukaza
- Mabadiliko katika mkojo na uvimbe
wa miguu na vifundoni
- Kukosa pumzi, maji kujaa katika
mapafu
- Shinikizo la damu (presha) bila
kua na uwezo wa kudhibiti
Ugonjwa sugu wa figo unaweza kuathiri karibu kila sehemu
ya mwili. Athari ni pamoja na:
- Kuhifadhi majimaji (Fluid
retention)
- Kupanda ghafla kwa potasium katika
damu
- Mifupa dhaifu, hatari ya mipasuko
kwenye mfupa na upungufu wa damu
- Kupunguza hamu ya tendo la ndoa
au kupoteza uwezo kabisa
- Uharibifu wa mfumo wa fahamu
- Kupungua utendaji wa kinga ya
mwili, ambayo inafanya kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi
Matibabu
Matibabu yana hatua mbali
mbali za kusaidia kudhibiti dalili, kupunguza athari, na kupunguza kasi ya
maendeleo ya ugonjwa huo. Kama figo likiwa limeharibiwa vibaya, mtu atahitaji
matibabu ya hatua za mwisho ya ugonjwa wa figo.
Namna ya kujikinga
- Pata tiba yashinikizo la damu
- Tiba ya kupunguza kiwango cha
cholestrol.
- Dawa za kutibu upungufu wa damu.
Dawa ili kupunguza uvimbe
- Tiba ya kulinda mifupa.
- Kupunguza ulaji vyakula vyenye
protini ili kupunguza taka katika damu.
Matibabu kwa hatua za mwisho wa ugonjwa wa figo
Katika hatua za mwisho wa ugonjwa
wa figo, matibabu ya kitaalamu yajulikanayo kama “dialysis” au kupandikiza figo
hunahitajika. “Dialysis” hasa huondoa bidhaa taka na maji ya ziada katika damu
wakati figo haiwezi tena kufanya hivi. Katika “hemodialysis”, mashine huchuja
taka na majimaji ya ziada katika damu. Katika “peritoneal dialysis”, mrija
mwembamba (catheter) uingizwa katika tumbo kisha kujazwa na majimaji yanayo nyonya
uchafu. Baada ya muda majimai haya yatoka mwilini yakibeba uchafu huo.
Upandikizwaji wa figo
Upandikizaji unajulikana kama "Zawadi ya
Maisha" kwa sababu inaokoa maisha na kurejesha ubora wa maisha kwa wale
ambao wamekuwa wagonjwa kwa muda mrefu. Upandikizaji una faida nyingi, hupunguza
haja ya “dialysis” na husaidia wagonjwa kufurahia maisha na kuwa huru zaidi.
Ingawa wagonjwa wengi hufanyiwa dialysis kabla ya uchunguzi zaidi kwa
upandikizaji, wagonjwa katika hatua za mwisho za ugonjwa wa figo wanaweza
kufanyiwa upandikizaji hata kabla ya kuanza “dialysis”.
Mafanikio katika upandikizaji wa figo hutibu
na kurudisha afya katika viungo hivo. Pamoja na hiyo huleta afya na maisha bora
ndio maana ni matibabu yanayopendelewa na wagonjwa wengi. Kawaida kutakuwa na
vizuizi vichache juu ya unywaji wa vinywaji na chakula baada ya kufanyiwa
upandikizaji. Wagonjwa wengi pia hurudi kufanya kazi na kuishi maisha kamili
baada ya operesheni hiyo..
Jinsi ya kuzuia Kushindwa
kwa figo
- Udhibiti wa ugonjwa wa kisukari na
shinikizo la damu
- Kupunguza ulaji wa mafuta na chumvi
·
Kufanya mazoezi kila siku za
wiki
- Kufanya uchunguzi wa mara kwa
mara
- Kuzuia utumiaji wa tumbaku
- Kuzuia utumiaji wa vilevi
- Kuepuka utumiaji wa dawa pasipo
maelekezo ya daktari
Dr Kavita Parihar ni
mtaalamu katika magonjwa ya figo amepata mafunzo ya magonjwa ya figo na upandikizaji figo kutoka taasisi maarufu
India, ana uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini. Alianzisha idara ya magonjwa ya
figo na programu ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad,
India mwaka 2003. Hivi sasa yeye ni kiongozi wa idara ya magonjwa ya figo na kupandikiza figo katika Hospitali ya
Apollo, Ahmedabad.
Dkt.
Kavita Parihar
MBBS,
MD (Medicine) DNB (Nephrology)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)