Dar es Salaam: Umakini kwa mara nyingine tena umewekwa katika
uhitaji wa wataalamu zaidi na kuboresha miundombinu ndani ya sekta ya utabibu
wa upasuaji wa mfumo wa fahamu. Hii inakuja baada ya ziara ya hivi karibuni na
timu ya madaktari kutoka hospitali ya Apollo nchini India. Madaktari ambao
walikuwa nchini kwa lengo la kujenga uhusiano unaoendelea kati ya hospitali
hiyo na Tanzania, walipata fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali ikiwa ni
pamoja na maboresho ya ujuzi wa wauguzi ambao walipata mafunzo kutoka hospitali
ya Apollo.
Matibabu
ya magonjwa ya mfumo wa fahamu ni mada nyeti yenye matatizo mbalimbali kama yakifanyika
kwa namna isiyo sahihi. Kuvurigika kwa mishipa ya fahamu ni ugonjwa ambao
unatokea katikati na pembeni ya mfumo wa neva. Ambapo kimuundo, upungufu wa bio-kemikali
au umeme kutokuwa sawa katika ubongo, uti wa mgongo au mishipa mingine na
inaweza kusababisha dalili za aina mbalimbali.
Tanzania
kwa sasa kuna madaktari wa mfumo wa fahamu 7 jumla ambao wote kwa sasa ni
watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Aidha tofauti
wenzao wa nchini India ukosefu wa data za kutosha kunamaanisha haiwezekani kuwa
na muonekano sahihi wa madhara ya maradhi ya mishipa ya fahamu kwa Watanzania
kwa ujumla. Akizungumzia hili Prof Dkt
Krishna Kambadoor Mkurugenzi wa Taasisi ya sayansi ya mfumo wa fahamu kutoka
Hospitali ya Apollo ya Bangalore
alisema kuwa hali ya sasa inaweza kukadiriwa kutoka takwimu za India na
kujifunza. Kulingana na nguvu ya idadi ya watu na mfanano wa magonjwa ya India
na Tanzania (ukiondoa magonjwa ya kuambukiza) mfano unaweza kupatikana.
Baada
ya kuthibitisha na watendaji wa Tanzania Prof
Dkt Krishna alikuwa na uwezo wa kuonyesha mambo mawili ambayo ni ya muhimu
kuyatazama kwa ajili ya baadaye, haya ni tabia za ulaji za watu pamoja na
ongezeko la umri wa kuishi wa watu kwa ujumla. Mlo usio kamili husababisha kesi
nyingi za magonjwa ya kisukari na matatizo yanayoambatana katika sehemu za
mwili ikiwa ni pamoja na kupoteza ufahamu (neurocognitive dysfunctions). Ambapo
tunaweza kuipongeza sekta yetu ya afya kwa ongezeko la hivi karibuni la umri wa
kuishi ni lazima pia kuangalia upande wa pili wa sarafu na kushughulikia
matatizo mbalimbali ambayo ni uhakika wa kufanya madhara. Matatizo haya ni
pamoja na kuongezeka idadi ya magonjwa yanayohusiana na umri mkubwa miongoni
mwao yakiwemo, mishipa ya fahamu na moyo kwa ujumla.
Ujio wa
madaktari pia ulikuwa sehemu ya mipango ya Apollo ya uliotazamiwa katika
kuendeleza sekta ya sayansi ya mfumo wa fahamu Tanzania. Hii ni hatua ambayo itatazama
utengenezaji wa vituo mtaalamu ambapo ita boresha huduma na kuongeza wataalamu
wa afya hapa nchini. Hospitali za Apollo zinatazamia kuleta zaidi ya miaka 20
ya maendeleo ya teknolojia na Prof Dkt
Krishna anasema kuwa "India kama
Tanzania ilikuwa katika hali kama hii miongo 3 iliyopita na tangu wakati
imeingia kutoka taifa linaloendelea na kuwa karibu sawa na taifa lililoendelea".
Anasisitiza kuwa "kwa juhudi za pamoja
kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi binafsi na serikali basi
Tanzania kwa upande wa matibabu inaweza kufikia ukuaji ulioonekana India kwa
miaka 20 na zaidi, katika muda wa miaka 5".
Uhusiano kati ya hospitali za
Apollo na Tanzania umekuwa na matunda kwa muda mfupi wa muongo mmoja. Mipango
inayopendekezwa itakuwa muhimu katika maendeleo ya miundombinu ya sekta ya
afya. "kwa kuwa huduma za afya si
kama huduma za gari ambapo baada ya uchunguzi yanaachiwa tu, upatikanaji wa
teknolojia ya kisasa na utaalamu utahakikisha uwepo na kuendelea kwa mchakato
wa huduma ajili ya wagonjwa" alihitimisha Prof Dkt Krishna.
Katika siku chache zijazo hospitali za Apollo zina
mipango ya kambi ya matibabu mwisho wa mwezi wa Machi, hii itaruhusu watu kuwaona
madaktari kwa ushauri juu ya maradhi mbalimbali. Kazi ambayo ipo katika hatua
za kukamilika itakuwa pia kama jukwaa kwa ajili ya kukusanya data ambazo
zitatoa picha ya hali ya sasa ya magonjwa yanayohusiana na mishipa ya fahamu
ndani ya nchi.
Kuhusu Hospitali za Apollo
Idara ya Magonjwa
ya mfumo wa fahamu ya Hospitali ya Apollo inawekwa kati ya hospitali bora
katika nchi. Wigo wa idara hii ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya magonjwa
yanayoathiri ubongo, uti wa mgongo, misuli na mishipa ya fahamu.
Uchunguzi wote wa magonjwa haya ujulikanao kitaalamu kama “EEG”, “video
telemetry”, “electromyography”, “stimulators magnetic” na vichochea uwezo vinapatikana
katika vituo hivi. Vifaa hivyo ni pamoja na “MRI Scan” na “MR angiography”, “CT
Scan” ya mfumo wa fahamu, “angiography” na “SPECT” ya kawaida.
Vidonge tiba kwa wagonjwa wa kiharusi na “botulinum toxin
therapy” kwa ”focal dystopia” hutumiwa na madaktari wakati
muhimu. Wapasuaji wa mfumo wa fahamu mara kwa mara hufanya upasuaji wa kichwani
na mgongoni, “stereotactic” bayopsi ya uvimbe “deep-seated” na “stereotactic radio surgery” kwa ajili ya matibabu ya ulemavu “artereovenous”
na uvimbe. “Aneurysms”, ulemavu wa mishipa na kichwa & shingo fuvu upasuaji
wake pia hufanyika katika hospitali ya Apollo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)