Mh. Shy rose Bhanji mgeni rasmi usiku wa Lady in Red 2015
..Kufanyika Nyumbani Lounge Ijumaa Februari 13
Na Andrew Chale
MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh. Shy rose Bhanji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye usiku maalum wa Lady In Red 2015, Ijumaa ya Februari 13, kwenye ukumbi wa M.O.G Bar (Zamani Nyumbani Lounge) huku mitindo ya nguo nyekundu zitauzwa kwa ajili ya siku ya wapendanao ‘Valentine day’.
Mwaka huu ni wa 11, tokea kuanzishwa kwa Lady in red, ambapo itajumuisha wanamitindo mbalimbali pamoja na wabunifu tofauti katika redcapert iliyotayarishwa maalum kwa ajili ya usiku huo.
Kwa mujibu wa wandaaji wa Usiku huo wa Lady in red 2015, Asia Idarous Khamsin ‘Mama wa Mitindo’ akishirikiana na Fashionnews Tanzania, alieleza kuwa usiku huo utapambwa na Gusa Gusa Min Band, kundil la Ngoma za asili na wengineo.
“Ijumaa ya Februari 13 ni siku maalum ya usiku wa Lady in red. Kwa kiingilio cha sh 10,000 kawaida na sh. 20,000 kwa upande wa V.I.P. Nguo nyekundu za Valentine day zitauzwa sambamba na kufurahia burudani mbalimbali” alisema Asia Idarous na kuongeza kuwa vazi maalum la usiku huo ni rangi nyekundu na tiketi za usiku zinapatikana Fabak fashions, Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere na Kobaz shop, Nyumbani Lounge.
Aidha, usiku huo wa Lady in red 2015, mdhamini mkuu ni Maji Poa, wengine ni Darling hair, , Vayle Spring, Eventlite, michuzi media group, chaneli ten, magic fm, sibuka tv, profile and style, Jambo Leo, mashughuli blog, vijimambo blog, Voice of America, Mo blog, Supernewstz blog na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)