Tarehe
4 ya mwezi wa pili, inatukumbusha kwamba tunapaswa kupambana na ugonjwa wa
saratani, ambao ni tatizo kubwa sana duniani kwa sasa. Mwaka huu, siku hii
maalum imepangwa kufikia matokeo chanya juu ya vita dhidi
ya saratani, kupitia kauli mbiu inayosisitiza kuwa ufumbuzi wakutokomeza
saratani upo ndani ya uwezo wetu. Kampeni ya mwaka huu 2015, Siku ya Saratani
Dunia inalenga katika kuchagua kudumisha maisha yenye afya, kutoa, upimaji kwa
wakati, tiba kwa watu wote na kuongeza ubora wa maisha.
Kulingana
na repoti ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ya January 2014. Takwimu zinaonesha, kuna wagonjwa mia moja (100)
wapya katika kila idadi ya watu laki moja (100,000). Hii
inamaanisha kuwa kila mwaka nchini Tanzania kuna wagonjwa 44,000 wapya wa
saratani nchini, kulingana na hesabu ya sensa ya mwaka 2012 kwamba Tanzania ina
takriban watu 44,900,000.
Kwa
mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanawake wapatao 7,515 kuugua
saratani ya kizazi, nchini Tanzania kila mwaka na 6,009 wanawake wanakufa
kutokana na ugonjwa huo. Saratani ya kizazi
inawakilisha 55% hadi 65% ya kesi zote za saratani kwa wanawake na 35% na 40%
ya kesi zote za saratani kwa ujumla. Saratani ya kizazi na saratani ya matiti
huwapata sana wanawake. Saratani ya Kaposi sarcoma,
ikifuatiwa na saratani ya umio, kichwa na shingo, huwapata sana wanaume. Pia
kuna ushahidi kwamba saratani ya tezi dume inakuwa kwa kiasi kikubwa sana. Vifo
pamoja na kesi hizi mpya za kansa zinahitaji kuzuiliwa.
Siku
ya Saratani Duniani inasimama kama jukwaa pekee ambalo linahamasisha na
kuongeza uelewa wa matokeo na athari zitokanazo na ugonjwa huu. Hivyo,
kuna mengi ya kufanywa nchini Tanzania na watu binafsi, jamii na serikali, kwa
kuunganisha na kuhamasisha ufumbuzi huu na kuchochea mabadiliko chanya.
Katika
kuadhimisha siku hii, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imeanzisha
kampeni ya ufahamu juu ya kansa kutoka tarehe 2 hadi 5 Februari. Kwa mujibu wa
mjumbe wa kamati ya kampeni ya saratani Dk Chuwa "kampeni itahusisha
uchunguzi wa bure wa saratani kwa watu Februari 4, 2015 katika taasisi hiyo’’
Taasisi
ya kimataifa mashuhuri kwa matibabu, Hospitali ya Apollo itakuwa mwenyeji wa warsha
ya siku moja Alhamisi, Februari 5 juu ya
Upasuaji kwa kutumia Roboti, upandikizaji wa uboho (BMT) na mambo mengine
muhimu yahusianayo na ugonjwa wa saratani katika hosipitali ya kansa ya Apollo,
Hyderabad. Ikifuatiwa na mkutano ujulikanao kama Apollo Cancer Conclave and Cancer CI 2015 (Mkutano wa
Kimataifa juu ya kutibu saratani, Elimu na Utafiti juu ya kansa) kutoka tarehe
6 hadi 8 February mwaka 2015 mjini Hyderabad”. Kwa kawaida
mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka miwili. Kati ya wajumbe 1800-2000 kutoka
India na nchi nyingine watashiriki.
Mkutano
utakuwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Saratani, Union for International Cancer Control
(UICC) na Umoja wa tiba ya kansa wa Ulaya, European Society for Medical Oncology
(ESMO). Majadiliano juu ya maendeleo mbalimbali katika teknolojia
katika tiba ya saratani, tiba ya mionzi kutoa mbinu na ushahidi juu ya tiba ya
saratani kwa ujumla.
Hospitali
ya Apollo inaongoza vita dhidi ya sarati katika njia nyingi kama vile mipango
ya kudhibiti mapema, elimu, kujenga ufahamu, makambi Tiba na Tiba, teknolojia
ya kisasa, wataalamu wakubwa, bodi ya uvimbe na huduma ya kina, ikiwa ni pamoja
upasuaji na ushauri. Wagonjwa wengi kansa huhisi mwisho wa maisha yao umefika
pindi wanapogundulika kuwa na ugonjwa huu. Habari njema
ni kwamba kansa inatibika, na lazima walau kutibiwa na mbinu jumuishi,
upasuaji, mionzi, ambazo zinapatikana katika Apollo Hospital.
Wakati
tukiadhimisha siku hii maalum waathirika wa kansa kutoka Tanzania ambao
walitibiwa katika Hospitali ya Apollo wametoa shukurani zao za dhati kwa
hospitali ya Apollo kwa kuweza kuwatibu ugonjwa huo. Bi Dina
Pauline Bina, alitembelea Hospitali ya Apollo kwa ajili ya matibabu ya kansa
alitibiwa na kupona kabisa. Anasema kwamba "Ni
vizuri kwamba mtu alifikiria uwepo wa hospitali kubwa kama hii, kwa kuwa
inasaidia sio tu watu wa India lakini pia nchi nyingine za Afrika. Katika
maeneo mengine ambapo hakuna aina hiyo ya hospitali watu wengi wanakufa si kwa
sababu wanapaswa kufa kwa wakati huo, lakini kwa sababu hawana huduma za afya
zinazoweza kukabiliana na hali zao’’.
Anaongeza
kuwa, "Kila siku nyumbani na familia yangu tunamshukuru Mungu kuwa
nilipewa nafasi ya pili katika maisha na hii iliwezekana kupitia hospitali ya Apollo"
Mume wake pia ametoa maoni juu ya uzoefu mzuri walioupata wakiwa hospitali ya Apollo. Aliongeza,
"Madaktari wako makini, wenye nia ya dhati, na wana ujuzi katika huduma
mbalimbali za matibabu maalum. Huduma
za wauguzi ni nzuri sana na vyumba vya hospitali vinawekwa katika hali ya usafi
na usalama."
Mgonjwa
mwingine aliyepona ugonjwa wa kansa ya kansa ya damu, kutoka Tanzania Bi.
Zuhura Shaban Luzilla, anatoa shukrani zake kwa Dr. Ranjan Kumar Mohapatra, Mtaalamu
katika hospitali ya Apollo, na Bibi Gathi kwa ajili ya kutoa huduma nzuri na
sasa amerejea kwenye afya yake ya kawaida.
Dk
Emmanuel Kandusi, Mwenyekiti na mwanzilishi wa Kampeni ya 50 Plus nchini Tanzania aliyepona saratani ya tezi dume. Alikuwa
akiteseka kutokana na ugonjwa huo kwa muda wa miaka kadhaa, baadaye alihamishiwa
hospitali ya Apollo na kutokana na maendeleo na upatikanaji wa vifaa muhimu na
wafanyakazi, yeye ulihudumiwa vizuri na kwa mafanikio. Sasa yeye ni
kiongoza wa kampeni ya saratani ya tezi dume.
Pamoja
na ukweli kwamba wengi wa Tanzania wamegundulika na saratani, imekuwa ikipuuziwa
na watu binafsi, jamii na Serikali juu ya umuhimu wa kuangalia afya zao mara
kwa mara kutokana na hofu kwamba hakuna tiba ya saratani. Ugonjwa
huu upo ndani ya uwezo wetu, tunaweza kupambana nawo.
Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali
ya Apollo imefanikiwa kupata kibali cha bodi ya Kimataifa((JCI) iliyopo Marekani bodi yenye lengo la kuboresha
ubora wa huduma ya afya na usalama duniani kote. Kibali cha
kimataifa cha dhahabu kwa ajili ya hospitali. Tofauti ya
kipekee ya kufikia kibali kwa ajili ya hospitali hiyo kuanzia Delhi, inakuwa
hospitali ya kwanza nchini India kupata vibali hivyo mfululizo kwa mara ya nne,
wakati hospitali ya Apollo Chennai, ikiwa hospitali ya kwanza kusini mwa India kupata
kibali hiki cha kipekee.
Hospitali
hii ni kituo bora katika huduma za saratani. Ina mtandao wa tiba ya kansa ambao
ni mtandao mkubwa sana nchini India. Unaotoa huduma ya Saratani
ikiwa ni pamoja na kinga na tiba . Yenye vifaa na hali
nzuri ya teknolojia kama vile upasuaji wa kwa kutumia Roboti, PET CT Scanner, Tumour
board na hivi karibuni wameongeza NovalisTx, kiwango kipya katika tiba ya
mionzi na upasuaji, Inatoa huduma ikiwa ni pamoja na mionzi ya saratani, madawa
ya saratani, upasuaji, pamoja na Kliniki ya kitaalamu kwa ajili ya saratani ya
matiti, Saratani ya kichwa, mdomo na koo.
Uchunguzi
wa wakati ni muhimu kwa mafanikio ya tiba, hospitali ya Apollo inatoa huduma ya
uchunguzi wa Saratani, ambayo ni pamoja na uchunguzi maalum wa kijinsia unaogusa
saratani zote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)