SIDO latoa Mikopo kwa wajasiliamali mkoani Iringa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIDO latoa Mikopo kwa wajasiliamali mkoani Iringa

 na fredy mgunda,iringa

SHIRIKA la kuhudumiaviwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 229.9 kwa wajasiriamali wa mkoa huo, katika kipindi cha July mpaka Desembea mwaka jana. Akizungumza na uhuru,  Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupata mitaji, na kuinua uchumi wao ili waondokane na umaskini.


Alisema mikopo hiyo ilitolewa kwenye vikundi mbalimbali vya  wilaya zote za mkoa wa Iringa na wajasiriamali mmoja mmoja, ambao  kupitia SIDO  wamefanikiwa kiuchumi. “SIDO imekuwa ikitoa mikopo kwa wajasiriamali kwa masharti naafuu tofauti na taasisi nyingine  za kifedha ili na riba ndogo ili kukuza mitaji yao, ”alisema.


Alisema lengo la kutoa mikopo hiyo, ni kuwasaidia  wajasiriamali na wananchi wasiokopesheka kwenye mabenki na taasisi nyingine za kifedha.


Alisema mikopo hiyo ni rahisi zaidi kwa vikundi kwa madai kuwa wanachama wamekuwa wakidhaminiwa na vikundi vyao, ambavyo ikiwa mwanachama huyo atakimbia basi kikundi hicho kitabeba mzigo wa kumlipia.


Alitaja changamoto kubwa inayowakabili hasa kwa wajasiriamali wa mijini kuwa ni kutorejesha mikopo yao, jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa SIDO na kuwafanya wengine wasikopeshwe fedha hizo.

Hata hivyo alisema kuwa mbali na mikopo hiyo, SIDO imekuwa ikitoa mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali, ili iwe rahisi kwao kufanya biashara kwa utaalam na kuweza kukuza biashara zao.


“Pamoja na mikopo tumekuwa tukitoa mafunzo kwa wajasiriamali  wetu na kuwawezesha kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi, ili kutanua uelewa wa biashara zaidi,”alisema Mahinya. Hata hivyo aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika

kufanya kazi na SIDO ili waweze kuondokana na ugumu wa maisha ambao
umekuwa ukiwakabili kwa kuamua kuwa wajasiriamali. Alisema ikiwa vijana watajikita kwenye ubunifu wa biashara, itakuwa rahisi kuaminiwa na SIDO na hatimaye kupatiwa mikopo midogo  midogo inayoweza kuwafikisha kwenye hatua ya kukopesheka na taasisi  


nyingine.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages