MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir aendelea na ziara yake ya siku mbili kanda ya ziwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir aendelea na ziara yake ya siku mbili kanda ya ziwa

Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha Kanda ya Ziwa, Lugaano Kasambala, akimpa pole Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, aliuawa mkoani Mwanza, hivi karibuni. Mama huyo anatibiwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kupata mareraha katika tukio la kuvamiwa na kuporwa mtoto wake. Kulia kwa Kasambala ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani waliyeambatana katika safari hiyo kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir kwa ushirikiano na Taasisi ya Kifedha, inayojihusisha na mikopo yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania, walifanya ziara ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea familia mbili zilizopoteza watoto wao wawili ambao ni walemavu wa ngozi.

Familia hizo ni ya Ester Jonas, mama wa marehemu Yohana Bahati na ile ya Sofia Juma mama wa mtoto Pendo Emmanuel, wote wakiwa ni watu wenye ulemavu wa ngozi, huku familia zote mbili zikipewa Sh Milioni 2 kila moja.

Akizungumza katika safari hiyo, Mbunge Shaimar alisema ameendelea kusikitishwa na mauaji hayo ya albino yanayotoa haki ya kuishi ya watu wote wenye ulemavu wa ngozi, huku akiitaka jamii kuacha kufavya vitendo hivyo visivyokuwa vya kiungwana kutokana na kudhulumu haki za kuishi za binadamu wenzao.


“Naumia juu ya vitendo hivi kwasababu na mimi nipo kwenye kundi hili lawatu wenye ulemavu wa ngozi wanaoendelea kupukutika siku hadi siku, hivyo tupambane na majangili haya, maana najua Mheshimiwa Rais, Dr Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamekuwa wakiguswaa mno na matukio haya yanayoichafua nchi yetu,' alisema Shaimar, ambapo pia aliishukuru taasisi hiyo ya kifedha kuingia katika harakati za kupambana na mauaji ya albino nchini Tanzania.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa taasisi moja ya kifedha, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.

Naye Meneja Mauzo wa wa taasisi moja ya kifedha Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema taasisi yao imeguswa na mauaji hayo na kuitaka jamii kushirikiana na viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana vikali na watu wanaoendeleza kufanya unyama wa kuteka watu wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu wanazojua wenyewe.

Alisema hali hiyo waliamua kufanya safari moja na mbunge Shaimar ambaye kiuhalisia ni balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, huku akiamini kwa ushirikiano huo unaweza kupunguza au kuondosha kabisa vitendo hivyo vya mauaji ya albino yanayoendelea kushika kasi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.


Wengine waliombatana kwenye ziara hiyo ni pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii Mwanza, Leah Linti, Katibu Tawala Msaidizi Crecencia Joseph, Mweka Hazina wa Chama cha Albino Taifa (TAS), Abdullah Omari, Jeshi la Polisi wilayani Misungwi, huku safari zote zikiwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanzaa, Magesa Mulongo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages