Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Abbass Talimba (kushoto) akikabidhi leseni kwa VIongozi wa Kampuni ya Murhandziwa ambao ndio wamepewa kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa nchini Tanzania.Aliyeshika Leseni hiyo ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece.
Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton - Masaki.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
TAARIFA YA PROF BONGANI AUG KHUMALO
(MWENYEKITI WA GIDANI INTERNATIONAL (PROPRIETARY)LIMITED NA MURHANDZIWA LIMITED
KATIKA HAFLA YA KUPOKE LESENI YA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE NCHINI KUTOKA
TAASISI YA SERIKALI INAYOSIMAMIA MICHEZO YA KUBAHATISHA NCHINI
TANZANIA (2 FEBRUARY 2015, DAR ES SALAAM, TANZANIA)
Leo tunashuhudia ujio wa kampuni ya pili kwa ukubwa
barani Africa inayojishughulisha na
michezo ya kubahatisha ikitangaza kuanza kutoa huduma zake hapa nchini.
Ujio wa kampuni hii unategemewa kuleta manufaa kwa nchi ya Tanzania na watanzania kwa ujumla
waliopo katika sekta rasmi na waliopo
katika sekta zisizo rasmi yaani wafanyabiashara
binafsi.Shughuli zitakazofanywa na kampuni hii zitaingiza fedha nyingi za
kigeni kwa serikali ambazo tuna imani zitatumika kuboresha maendeleo ya nchi na
huduma kwa wananchi wake.
Kampuni ya Murhandziwa
mbali na kunufaisha wananchi kupitia mapato yatakayolipwa serikalini pia
itatoa ajira kwa watanzania wengi na wengine wengi watanufaika kwa kufanya
biashara na kampuni hii kwa kutoa huduma
na kuiuzia mahitaji mbalimbali.
Tutaanzisha maduka mbalimbali ambayo yatakuwa yanaendesha michezo mbalimbali ya kubahatisha
na ambayo pia yatakuwa yanauza tiketi za kushiriki kwenye
michezo ya kubahatisha tutakayokuwa tunaendesha na tumejipanga kutokana na
uzoefu wetu kuhakikisha tunaboresha huduma hizi kama ilivyo katika nchi
mbalimbali duniani na kuthibitisha kwamba sekta hii ni moja ya sekta inayoweza
kuchangia pato la taifa na kukuza uchumi kwa kiasi kikubwa.
Kampuni ya Gidani
International (Proprietary) Limited ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya
Murhandziwa Limited ili kuendesha
shughuli zake kwa ufanisi nchini
imejipanga kuwapatia ujuzi wa aina mbalimbali watanzania itakaowapatia ajira
kuhusiana na fani ya michezo ya kubahatisha ambao yatatolewa na wataalamu waliobobea katika fani hii kutoka nchi
mbalimbali duniani.
Vilevile kampuni hii inatarajia kuwa katika kipindi chote itakachokuwa inatoa
huduma nchini itawawezesha watanzania wataoshiriki michezo mbalimbali itakayoiendesha
kuwa mamilionea na imejizatiti kutoa huduma bora kwa washindi na washiriki wa
michezo itakayokuwa inaendesha ikiwemo kuwashauri jinsi ya kufanya uwekezaji wa busara kwa fedha watakazojishindia.
Kampuni ya Gidani International siku zote itakazokuwa
inatoa huduma nchini itakuwa makini kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na sheria elekezi kutoka
Bodi ya Serikali ya kusimamia michezo ya kubahatisha ambayo iko kwaajili ya
kuhakikisha michezo hii ya kubahatisha inaendeshwa kwa misingi ya sheria,usawa
na bila udanganyifu wowote.
Tunaamini kuwepo kwa michezo hii kuwa ni moja ya sekta
inayoshiriki katika kukuza uchumi wa
nchi na kupambana na janga la kuondoa
tatizo la umaskini kwenye jamii,na ndio maana serikali imekuwa ikitoa kibali cha
kufanyiika michezo hii na ina bodi inayoratibu uendeshwaji wake nasi tukiwa
wadau tutafanya kazi kwa karibu na serikali na vyombo vyake ikiwemo wananchi wa Tanzania ambao watakuwa wadau
wakubwa wa michezo hii.
Tumefurahi kuja hapa nchi tukijua uhusiano mkubwa uliopo
baina na Tanzania na Afrika ya Kusini katika Nyanja mbalimbali na tunaamini
ujio wetu unazidi kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi
mbili,kuzidi kuimarisha pia Muungano wa nchi za Afrika.Kwa kuzingatia hilo
tutaheshimu sheria zote za nchi na kuendesha shughuli zetu kwa umakini na
weredi mkubwa na kuhakikisha zinaleta manufaa kwetu sote.
Sekta ya michezo ya kubahatisha nchini itabadilika kwa
muda mfupi na kutambulika barani afrika kutokana na uwekezaji wa kiteknolojia
tutakaoufanya.Tunajivua kuwa miundombinu
na vifaa vyetu vya kuendesha michezo hii ni vya kiwango cha juu
vilivyotengenezwa hapa hapa barani Afrika.Vituo 4,000 vya michezo na mauzo ya
tiketi na vifaa vingine vya kisasa
vinavyohamishika zaidi ya 1,000 vitaletwa
hapa nchini hivi karibuni kwa ajili ya kuzindua huduma zetu.Tutaanza
kuuza tiketi Julai 4 ambapo ndipo utafanyika uzinduzi rasmi.
Neno murhandiwa ni la lugha ya Tsonga moja ya lugha kubwa
katika ya lugha 11 zinatotumiwa na watu wengi nchini Afrika ya Kusini likiwa na
maana ya “Mpendwa wako”.Nina imani kubwa kuwa Murhandziwa itapendwa katika kila
familia na wananchi wote wa Tanzania kwa ujumla.
Mwisho
Imetolewa na Prof Bongani Aug Khumalo
Mwenyekiti
Imetolewa na Prof Bongani Aug Khumalo
Mwenyekiti
Gidani International (Proprietary) Limited
Murhandziwa Limited
Aggrey & Clifford
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)