Arsenal hoi dhidi ya Monaco UEFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Arsenal hoi dhidi ya Monaco UEFA


Wachezaji wa Arsenal
Matumaini ya Arsenal kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo imeingia nyongo hapo jana baada ya kubali kipigo nyumbani mbele ya mashabiki wao kutoka kwa Monaco ya Ufaransa cha mabao matatu kwa moja.
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Dimitar Berbatov ambaye naye alirejea England alikuwa ni miongoni mwa waliopachika magoli hayo kwa upande wa Monaco.
Huku magoli mengine yakipachikwa na Geoffrey Kondogbia na Yannick Ferreira Carrasco.
Goli la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Oxlade Chamberlain.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo Bayer Leverkusen ya Ujerumani ilipata ushindi wa bao kwa 0 dhidi ya Atletico Madrid. Goli hilo pekee la Bayern Liverkusen lilitiwa kimiani na Hakan Calhanoglu.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages