MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA CHINA NA UJUMBE WAKE IKULU DAR LEO, WASAINI MIKATABA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AMKARIBISHA MAKAMU WA RAIS WA CHINA NA UJUMBE WAKE IKULU DAR LEO, WASAINI MIKATABA

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku
sita
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake  wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
 Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages