PICHA YA HELIKOPTA YA JESHI ILIYOANGUKA WAKATI IKIWA IMEWABEBA MAKAMU WA RAIS,MH DKT BILAL, MKUU WA MKOA WA DSM,Mh MECKY SADIQ - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PICHA YA HELIKOPTA YA JESHI ILIYOANGUKA WAKATI IKIWA IMEWABEBA MAKAMU WA RAIS,MH DKT BILAL, MKUU WA MKOA WA DSM,Mh MECKY SADIQ

Helkopta iliyokuwa imewabeba baadhi ya viongozi wa serikali baada ya ajali.
Kikosi cha zimamoto kikiizima helkopta hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania iliyokuwa imewabeba viongozi  wa serikali.
MAKAMU wa Rais Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na mpiga picha wa TBC, George Kasembe wamenusurika kifo baada ya helkopta waliyokuwa wanasafiria kupata ajali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Viongozi hao walikuwa katika helkopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa ziara ya kukagua athari za mafuriko jijini Dar es Salaam.

Baada ya ajali, viongozi hao  wamepatiwa matibabu katika majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao!Credit GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages