WASHINIDI WA KUNUNUA FILAMU ZA PROIN KUIBUKA NA TV ZA SAMSUNG NA DEKI ZAKE KILA WIKI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASHINIDI WA KUNUNUA FILAMU ZA PROIN KUIBUKA NA TV ZA SAMSUNG NA DEKI ZAKE KILA WIKI.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions, Evance Stephen akionyesha stika ya TRA ambayo hudhihirisha uhalali wa kazi halisi ya wasanii Kutoka kampuni ya Proin Promotions ambayo itakuwa na namba za ushindi katika promosheni hiyo ya Kununua Filamu Halisi kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited ambapo Mshindi ataibuka na TV ya Samsung pamoja na Deki yake. Pembeni yake ni Meneja Mradi wa shindano la kusaka vipaji (Tanzania Movie Talent) Joshua Moshi.
..................................................
Proin Promotions Limited, Kampuni inayouza,kusambaza na kutengeneza filamu za kitanzania Imeanzisha Kampeni ya Kununua Filamu Halisi za Kitanzania kutoka Proin promotions na Katika kampeni hiyo Watanzania watakaonunua Filamu halisi za kitanzania kutoka Proin wataweza kujishindia Zawadi ya TV aina ya Samsung pamoja na Deki yake.

Ili kuweza Kushinda Zawadi unachotakiwa kufanya ni kununua filamu za Proin zenye stika maalumu ya TRA ambayo inakuwa na namba baada ya kununua hiyo FIlamu yenye Stika hizo za TRA, Kutakuwa na droo inatakayochezeshwa na Kampuni ya Proin Kwa Usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha na namba za stika zitakazo bahatika Kuibuka Mshindi, Kampuni ya Proin itatangaza Kwenye Vyomb vya Habari na Muhusika atatakiwa kufika katika Ofisi za Proin Na Vithibitisho vyake.

Washindi wa Promosheni hii watatangazwa katika Vyomb mbalimbali vya Habari, Blogs, Tovuti yetu ya http://www.proinpromotions.co.tz pamoja na Ukurasa wetu wa facebook wenye kiunganishi kifuatacho http://www.facebook.com/tztmt 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages