TFDA KUTEKETEZA VIPODOZI VISIVYOFAA VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 188 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TFDA KUTEKETEZA VIPODOZI VISIVYOFAA VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 188

Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na wanahaabari (hawapo pichani) kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka hiyo.Kulia ni Afisa  Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza, akionesha moja ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamalaka hiyo kinachotumiwa na wanawake kukuza makalio.
Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza (hawapo pichani). Picha na Hussein Makame MAELEZO.


Frank Mvungi-Maelezo

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imeteketeza vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya binadamu vyenye thamani ya takribani Shilingi Milioni 188 katika  kipindi cha mwaka 2012/2013.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza  wakati akizunguza na wanahabari kwenye mkutano na waandishi wa habari leo  jijini Dar es salaam.

Alisema TFDA imeweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia  njia mbalimbali ambazo ni pamoja na usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya  biashara ya bidhaa husika na ukaguzi wa majengo ya vipodozi.

Simwanza aliongeza kuwa hatua nyingine ni ufuatiliaji wa vipodozi katika soko  ili kujiridhisha kuwa vina ubora na usalama unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na  taratibu zilizowekwa.

Alibainisha kuwa vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu vina  madhara kama vile kusababisha kupata mzio wa ngozi, kusababisha ugonjwa wa ngozi kwa mtumiaji.

“Matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya zebaki (mercury) kwa mama
wajawazito huathiri mtoto tumboni hali inayoweza kusababisha madhara makubwa  kwa mtoto atakayezaliwa.

Alifafanua zaidi kuwa viambato kama Zirconium na Vinyl Chloride husababisha  kansa ya ngozi na mapafu kwa mtumiaji wa vipodozi vyenye kemikali. Simwanza alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha matumizi ya vipodozi vyenye viambata vyenye sumu na kemikali.

TFDA imekuwa ikifanya operesheni na ukaguzi wa vipodizi katika maduka

mbalimbali yanayouza bidhaa hizo na kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya  binadamu na kuziteketeza kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages