Picha Zilizoonyeshwa Kwa Satelite kuhusu mabaki ya ndege ya Malaysia Sio Yenyewe. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Picha Zilizoonyeshwa Kwa Satelite kuhusu mabaki ya ndege ya Malaysia Sio Yenyewe.


Picha za satelite za China
Maafisa wa Serikali ya Malaysia waliokuwa wanadadisi picha zilizopigwa na mtambo wa Satelite wa China ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyotoweka, Jumamosi, wamesema kuwa mabaki hayo yalitoweka na huenda sio mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka siku ya jumamosi .
Serikali ya Malaysia imesema kuwa picha hizo zilitolewa kwa bahati mbaya.
Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Amewaambia wandishi wa habari mjini Kuala Lumpar kuwa Picha hizo zilizopigwa siku ya Jumapili,saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka na abiria 239 zinadaiwa zilitolewa kimakosa na maafisa wa China.
Aidha tetesi kuwa kifaa cha kupeperusha matangazo cha ndege hiyo kimekuwa kikituma taarifa imesemekana kuwa si ukweli .
Waziri huyo amesema kuwa kupotea kwa ndege hiyo sio kitu kilichotararajiwa.
Picha hizo zilitolewa na idara ya serikali ya China ya sayansi na teknolojia siku ya Jumatano.
Bwana Hussein kadhalika amekanusha ripoti ya jarida la Wall Street kwambandege hiyo ilituma data ya Engine yake kwa karibu saa 4 kabla ya kupoteza mawasiliano na kituo cha trafiki ya ndege.
Amesema kuwa juhudi za kuisaka ndege ghiyo zingali zinaendelea.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages