TAIFA STARS KUTUMIA UZI WA ADIDAS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAIFA STARS KUTUMIA UZI WA ADIDAS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzan(TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.

Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek kama inavyoonekana pichani.

Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.

TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages