TAIFA STARS KUREJEA NCHINI KESHO MCHANA KUTOKA NAMIBIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAIFA STARS KUREJEA NCHINI KESHO MCHANA KUTOKA NAMIBIA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) saa 12.45 jioni kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.15 mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages