MOVIE REVIEW: MTAZAMO WANGU JUU YA FILAMU YA KITANZANIA IITWAYO NETWORK. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MOVIE REVIEW: MTAZAMO WANGU JUU YA FILAMU YA KITANZANIA IITWAYO NETWORK.

 
UTANGULIZI:
NETWORK ni moja ya filamu ya kitanzania iliyotengenezwa na Na Kampuni ya Kalage Pictures ambayo ipo chini ya Mkurugenzi wake John Kalage lakini Pia ikiwa inatoka Swahilihood.

Ni moja ya Filamu inayouzwa na kusambazwa na kampuni ya Proin Promotions Limited  ambapo Kwanza Inapatikana Kwenye Maduka Yote ya Kuuzia Filamu Nchini.

IFUATAYO NI MTAZAMO JUU YA UHALISIA WA FILAMU HIYO NA MAZINGIRA YA KITANZANIA:

Kwanza Kabisa Filamu hii ina uhalisia kwa Asilimia 90 ambapo kwa baadhi ya matukio yaliyomo kama Vile kulipiza Kisasi, Mauaji, Kuambukizwa Kwa Makusudi magonjwa ya Zinaa nk ni baadhi ya matukio tu yaliyopo katika Filamu hiyo, kiukweli matukio hayo yapo na yanatokea katika mazingira yetu tena sana tu na Kiuhalisia Kweli hii filamu ina uhalisia na sio Filamu ambayo ina matukio ya kusadikika.

JUU YA MCHANGANYIKO WA RANGI:
Kwanza kabisa nawapongeze Kalage Pictures kwa jinsi walivyoweza kujitahidi sana katika zoezi zima la Kutengeneza filamu hii na kuweza kuchanganya rangi vizuri na kupelekea kama Filamu hii ilitengenezwa kwa Kutumia Kamera za zamani ambazo ndio zinatoa rangi kama hii, kiukweli ni rangi ambazo unaweza kuzipata kwenye filamu za Zamani kutoka Hollywood yaani 1980s kwa hilo kajitahidi sana. Na Rangi zake ni Nzuri pia na zinavutia.

JUU YA WAHUSIKA:

Kwanza kabisa katika filamu hii Muhusika Mkuu ni Ni Muigizaji Mmoja aitwaye BRIAN IBRICK jina la kisanii alilotumia kwenye filamu hii anaitwa Detective (Mpelelezi) Demango, Huku akisaidiwa na VYONE CHERRIE wakati kwenye filamu hii anatumia jina la Detective Eliza (Monalisa huyo).

Hawa kweli waliweza kuuvaa uhusika haswa katika vipengele walivyoigiza kwanza Nimuongelee Detective Eliza kiukweli aliuvaa uhusika haswa pale katika kipengele cha kumkimbiza Kijana aliyekuwa akifanya biashara za magendo hadharani na walipomkimbiza kweli Detective Eliza Aliweza kuonekana akikimbia haswa pamoja na kutumia teknolojia kumuongezea mwendo lakini sehemu kubwa aliweza kukimbia na kuonyesha kuwa alikuwa fit kwenye kipande kile na jinsi alivyoweza kuigiza kama Mpelelezi

Nirudi kwa Mpelelezi Demango huyu yeye aliweza kabisa katika Kuonyesha Jinsi gani watu wanaweza kuwaambukiza wanawake kwa makusudi kabisa virusi vya ukimwi, na Vilevile kwa nafasi yake yeye kama Mpelelezi aliweza kuonekana ni mmoja wa Wapepelezi wenye uzoefu wa siku nyingi lakini aliyeshindwa kupata taarifa sahihi za Uhalifu mbalimbali wa mauaji yaliyoyokuwa yakitokea na wizi kwasababu ya kupokea rushwa na Haya yapo Kwenye jamii zetu....

Kiukweli waliweza kuuvaa uhusika haswa na kufanya filamu hii kuonekana yenye uhalisia zaidi kuliko matukio ya kusadikika.

JUU YA UTOFAUTI NA FILAMU NYINGINE ZA KITANZANIA:

Kwanza utofauti wake mkubwa ni Kuanzia rangi zilizotumika, zimetumika vizuri sana tofauti na filamu nyingine kuwa rangi zinakuwa zimechanganywa kama mtu amelazimishwa, Pili filamu hii imetengenezwa takriba miezi miwili tofauti na filamu nyingine zinatengenezwa ndani ya wiki kadhaa tu. Tofauti nyingine ni Sauti Kwenye sauti zinasikika vizuri kabisa japokuwa Kuna baadhi ya Matukio wameshindwa kuacha sauti halisi Mfano  Mpelelezi Demango wakati anaongea na simu huku akiendesha gari nilitarajia Kusikai Mlio halisi wa gari japo kwa mbali ilikuweza kuleta uhalisia wa tukio hilo.Vipo vingi sana vinavyoonyesha Utofauti na filamu nyingine.

JUU YA MFANANO NA FILAMU NYINGINE ZA KITANZANIA:

Hakika nimeshindwa kuelewa Kuwa Tasnia hii ya filamu Tanzania wameshindwa kabisa kutofautisha Muundo wa FIlamu zao maana Stori huwa nzuri lakini Sasa Unapoangalia Kipande kimoja unaweza kutabiri kipande kijacho baada ya kuona kipande cha Nyuma na Kikawa kama ulivyoweza kutabiri , Filamiu nyingi za Kitanzania unajua kabisa kinachofuata baada ya kipande hiki ni hiki "ABCD". Kwa hili Badilikeni Bongo Movie.

JUU YA MAPUNGUFU YA FILAMU HII:
Kama ilivyo ukweli usiopingika kuwa Sisi Binadamu hatujakamilika na Hakuna Kizuri kisicho na kasoro, Kasoro ni sehemu ya Maisha yetu lakini Kwa Asilimia Kubwa Kasoro niliyoweza kuziona ni Kama Vile kwenye kipande cha Mpelelezi Eliza alipokuwa akimuhoji Yule Kijana Ndani wakati wakiwaonyesha kwa Karibu wakiweza kuonyesha kabisa Kuwa Kulikuwa ni Usiku na Pembeni kulikuwa na giza lakini walishindwa kukumbuka kama waliweka Giza matokeo yake kipande hiko wakikionyesha kwa Umbali kidogo panaonyesha Chumba hiko kina Mwanga baadhi ya sehemu wakati mwanzo kulikuwa na giza.Kwa Hili rekebisheni kwenye movie nyingine msirudie kosa kama hilo,maana wengine huwa tunaangalia kwa umakini kama nini. Mapungufu mengine ni Kama Vile hatukuweza kusikia sauti halisi badala yake walipandishia sauti japokuwa walifanya vizuri sana kupandishia sauti na hawakuaribu kwasababu midomo na matamshi vilikuwa vinaendana haswa kwa hilo Big Up. Hayo ni Baadhi tu

HITIMISHO

Kwa asilimia 90 Ni filamu nzuri sana Hasa kabisa ikiwa inahakisi jina la Filamu na Matukio yaliyomo humo na vilevile ni filamu inayosisimua na Kuelezea Visa halisi kabisa vinavyotokea katika Jamii zetu zinazotuzunguka.

Pongezi kwa John Riber kwa Kusupport tasnia hii ya filamu na kuleta mabadiliko katika Tasnia hii ya Filamu Tanzania. Vilevile Pongezi kwa Kalage kwa kuweza kuitengeneza Filamu Hii haswa katika viwango vingine vya Juu zaidi, Mapungufu yapo lakini tuyafanyie kazi ili Kuweza kutoa kazi nzuri hapo baadae.

Shukrani kwa Proin Promotions Limited kwa Kusambaza filamu hii nchini.na Kuamua Kupokea kazi bora kabisa.

JIPATIE NAKALA YAKO SASA....

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages