
Bi. Gladness Nkya akikabidhi zawadi kwa wawakilishi wa Kituo cha Upendo Daima katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake ambapo badala ya kufanya sherehe ya kunywa na kula pamoja na marafiki ameamua kwenda kusheherekea na watoto yatima katika kituo hicho.

Gladness Nkya akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Upendo Daima.

Imekuwa hali ya kawaida
kwa watu mbalimbali hasa vijana kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa hafla
mbalimbali pamoja na marafiki ambapo hunywa vinywaji mbalimbali na kula vyakula
wakati mwengine mpaka kusaza lakini hilo limekuwa tofauti kwa mdau Gladness
Nkya ambae yeye ameona atue fursa ya siku hiyo kusheherekea pamoja na watoto
yatima wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo Daima kilichopo Nyegezi,
Malimbe karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino jijini Mwanza.
Unaweza kuona ni vitu
vidogo lakini moyo mkubwa aliokuwa nao Bi. Gladness katika kusaidia wengine
wenye mahitaji Zaidi yake ni kitu cha kuigwa na cha mfano kwa vijana wengine
ambao wana nafasi ya kuisadia jamii inayowazunguka. Wahenga walisema “Kutoa ni
Moyo na si utajiri”.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)