BONDIA FADHILI AWADH AFARIKI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BONDIA FADHILI AWADH AFARIKI


Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya Mwananyamala jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa siku kadhaa. 
Marehemu Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza  mpambano wa ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka Tanga Alan Kamote, na  alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo. 
Sababu ya kifo chake kwa ripoti ya daktari wa Mwananyamala kwa kiongozi wa ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadirika pale alipojaribu kufanya  mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. 
Fadhili awadh mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali. 
Shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.
Sisi tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi,
Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “Tiger” peponi 
 AMINA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages