Maelfu ya wakimbizi ambao wamekuwa wakitoroka nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita nchini humo wamehamia Uganda. Mpigaji Picha, Fredric Noy, anayefaifanyia kazi Idara ya wakimbizi ya Umoja wa mataifa, anatumia picha, kufarisia maisha ya ukimbizi ya Atem Angang na familia yake.
Mji wa Bor alimokuwa anaishi Matiop Atem Angang ndilo lililokuwa la kwanza kudhibitiwa na waasi pindi vita vilipozuka Sudan Kusini mnamo Desemba 15. Yeye pamoja na familia yake kubwa ya watu 15, akiwemo mamake wa miaka 95, watoto wake sita pamoja na familia ya dadake walitoroka kutoka nchini humo.
Lori linalowasafirisha wakimbizi kutoka Sudan, akiwemo Bw. Angang na familia yake, linavuka daraja kabla ya kufika kituo cha uhamiaji cha Dzaipi. Lori hizo husafiri hadi mara nne kwa siku kati ya mipakani na kituo hicho cha uhamiaji.Kwa Picha Zaidi BOFYA HAPA

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)