
Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII. Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.
Mzee Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30 katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia mitandao ya kiJamii.
Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada .Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine. Karibu sana
NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)