
Mpiga picha Bill Gekas kutoka nchini Australia, ametuzwa mara nyingi kwa picha zake nyingi na za kupendeza. Alijifunza mwenyewe sanaa hii kutokana na kuenzi picha za watu wa zamanai zilizompa motisha ya kuchora picha zake

Katika mradi wake ambapo anatoa mfano wake kutoka kwa wachoraji wajuzi wa Ulaya na waliochora mwaka 1800. Gekas amemtumia msichana wake mwenye umri wa miaka sita katika kila picha kuleta taswira hiyo ya waliokuwa watu wakubwa zamani

Hupanga vyema mavazi na taa wakati akipiga kila picha na kuzifananisha na picha za zamani kiasi. Picha hii yenye kichwa 'Doilies In Delft,' mchoraji wake ambaye aliitwa Johannes Vermeer alizaliwa Delft

Mchoraji huyo mashuhuri kutoka Uholanzi alichora picha 34 pekee maishani mwake. Moja ya picha zilizowavutia watu ilikuwa moja ya msichana aliyekuwa amevalia kipuli.

Picha nyingine nzuri ilikuwa ya msichana ambaye hakuvalia kipuli. Gekas aliipiga picha hii kwa kutumia taa mbili na vitambara vya nguo. Kwa Picha Zaidi Bofya Hapa





gud job
ReplyDelete