NEWS ALERTS:BOTI YA MV KILIMANJARO II KUTOKA PEMBA KUELEKEA UNGUJA YANUSURIKA KUZAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NEWS ALERTS:BOTI YA MV KILIMANJARO II KUTOKA PEMBA KUELEKEA UNGUJA YANUSURIKA KUZAMA


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema boti ya Kilimanjaro 2 iliyokuwa ikitoka Pemba kuelekea Ugunja inasemekana imepingwa na dhoruba kali na kunusurika kuzama, inadaiwa kuna vifo vimetokea.
Ukweli ni kwamba wimbi kubwa liliipiga boat na kusababisha hali ya tafrani. Nimetoka kuongea na mamlaka ya bandari sasa hivi na boat iko njiani inakuja unguja iko maeneo ya Beit ras sasa hivi. Haijazama  na iliondoka na abiria watu wazima 269, watoto 60 na mabaharia 8 wote wako salama.
Wimbi kubwa liliipiga likachukua mabegi na baadhi ya life jackets. Injini za boat zilizima, ilibidi watulie kwa muda kuona kama wimbi lilichukua na baadhi ya abiria lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeachwa.
Nakumbuka mamlaka ya hali ya hewa walitoa tahadhari kuhusu mchafuko wa bahari hizi siku.
 
Tunamshukuru mungu kwa kuepusha hili janga.

CHANZO: JAMII FORUM NA CLOUDS FM

1 comment:

  1. Anonymous5:24 PM

    all boats fron kendwa and nungwi went for rescue, found 4 people and 4 bodies. The survivors report about 50 more passengers are lost

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages