Mkurugenzi wa Purosangue Athletic Club, Bw. Nico Angelo Pannevis (kushoto) akimweleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumueleza mpango wa Klabu yake kushirikiana na Tanzania Kuwaendeleza Wanariadha chipukizi nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa Purosangue Athletic Club, Bw. Nico Angelo Pannevis (katikati) alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumueleza mpango wa Klabu yake kushirikiana na Tanzania Kuwaendeleza Wanariadha chipukizi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leonard Thadeo.
………………………………………………………………
Na Genofieva Matemu,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Serikali ya Tanzania kushirikiana na Wadau wa mchezo wa Riadha kuinua vipaji
Serikali ya Tanzania kwa kushirikana na wadau wa mchezo wa riadha kutoka nchini Italia imepania kuendeleza mchezo wa riadha ili kuinua vipaji vya wanariadha chipukizi nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Mkurugenzi wa Klabu ya Purosague Athelics ya Italia, Bw. Nico Angelo Pannevis alipomtembelea ofisini kwake.
Prof Gabriel amesema kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Wadau wa Mchezo wa Riadha ili kuhakikisha kuwa Wanamichezo chipukizi wanaendelezwa na kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa na Kimataifa.
Naye Bw.Pannevis ameeleza mpango wa Klabu yake wa kujenga kituo cha Mchezo wa Riadha hapa nchini ili kuwaendeleza Wanariadha chipukizi katika kuwajengea uwezo katika mchezo huo na fani nyingine za maisha.
Aidha, Bw. Pannevis amesema kuwa hapo baadae Klabu yake haitajikita tu kwenye riadha bali pia inalenga kuendeleza michezo ya walemavu ili kuwawezesha kufikia ndoto zao za kimichezo kama wanamichezo wengine.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)