RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MAZIKO YA MZEE NELSON MADELA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MAZIKO YA MZEE NELSON MADELA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana. PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serilai, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 

Kesho Novemba 11 hadi Novemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages