Mtoto Mtanzania ashinda insha EAC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mtoto Mtanzania ashinda insha EAC

Peter Robert Kilave (pichani), mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Tushikamane ya mjini Morogoro, amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika shindano la insha kuhusu ujenzi wa miundombinu Afrika Mashariki. 

Amepewa tuzo ya dola za Marekani 1,500 na cheti na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. 

Hiyo ilikuwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC jijini Kampala, leo Jumamosi, Novemba 30, 2013. Rais Jakaya Kikwete alimwita jukwaani na kumpa mkono wa pongezi huku ukumbi ukizizima kwa shangwe. 

Kijana huyo mtanashati na mpole alijizolea dola zingine kutoka kwa viongozi na maafisa wa Serikali ya Tanzania kwa kuibeba Tanzania katika kipindi hiki chenye changamoto za ajabu ajabu ndani ya Jumuiya.

Mshindi wa pili alitoka Uganda; wa tatu Burundi; wa nne Rwanda na Mkenya alishika mkia. 

Dogo huyo wa Tanzania ataendelea kuvinjari nchini Uganda kwa siku ili wamwone kwa karibu zaidi. Atakuwa na maafisa wa EAC, afisa mwandamizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Tanzania pamoja na mwalimu mkuu wake.

Hongera Watanzania wote.

Na mdau Matinyi

1 comment:

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages