Binti akiwa na mshumaa wakati wa ibada ya maombi ya kumkumbuka Nelson Mandela katika kanisa la Regina Mundi lililopo Soweto, Afrika Kusini leo.
Waumini wakiwa katika ibada ya maombi ya kumkumbuka Nelson Mandela katika kanisa la Methodist mjini Johannesburg leo. (Picha na Reuters)
Wananchi wa Afrika Kusini leo wanashirki maombi ya kitaifa ya kumkumbuka marehemu Nelson Mandela.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma atahudhuria maombi hayo katika kanisa la Methodist mjini Johannesburg, wakishirikiana na viongozi wengine kutoka dini mbalimbali kwa maombi yatakayofanyika siku nzima leo.
Maombi maalum ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumanne kabla ya kufanyika mazishi ya kitaifa Jumapili tarehe 15 Desemba mwaka huu.
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha tangu Mandela kufariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Rais Jocob Zuma amewataka wananchi kwenda katika viwanja vya michezo, makanisa, kumbi mbalimbali na sehemu zingine zote za maombi leo Jumapili, kumkumbuka Mandela.
"Wakati huu tunapoomboleza kifo cha Mandela, tunapaswa kuwa pia tunaimba kusherehekea maisha yake kwa juhudi za mageuzi alizozifanya na kutuletea maisha mapya, tumuimbie Madiba,’’ alisema Rais Jacob Zuma.
Mrithi wa Mandela alipoondoka madarakani, Thabo Mbeki, atahudhuria maombi katika kanisa ya Oxford Shul Synagogue mjini Johannesburg leo mchana.
Viongozi wengine wakuu wa ANC, watahudhuria maombi katika maeneo mengine nchini humo.
Chanzo: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)