"Kweli Bini ana Huruma" Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Bibi Geremana Mrwiro mwanakijiji ambaye alileta jembe ili litumike kwa kusaidia kunasua magari yaliyokuwa yamekwama kwenye tope
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging'ombe ambapo Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na kuendesha kilimo .
Baadhi ya vijana hao wakinyanyua kadi zao juu ili kula kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi kijana Said Mkweta.
Utulivu wa kula kiapo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi kuhuso moja ya Power Tiller itakayotumiwa na vijana hao kulimia shamba lao ili kuwahi mvua zinazonyesha.
Gari lililokuwa likitumiwa na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa likinasuliwa kwenye tope mara baada ya kuteleza na kuingia kandokando ya mtari
Juhudi za kunasua zikiendelea.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata kulia Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakitoka nje mara baada ya katibu mkuu huyo kuzindua jengo la kitegauchumi la CCM mkoa wa Njombe leo ambalo limepangishwa na Wizara ya Fedha.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-WANGING'OMBE-NJOMBE)
-





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)