Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, anatarajiwa kufunga pazia la maonesho ya Sita ya Swahili Fashion Week –SFW 2013, litakalohitimishwa usiku wa Desemba 8, jijini Dar es Salaam, katika hoteli ya Golden Tulip.
Akielezea juu ya onesho hilo , Asia Idorous ‘Mama wa Mitindo’ alipongeza wandaaji wa SFW 2013, kwa kufikia hapo kwani wameweza kuendeleza tasnia hiyo sambamba na kuibua vipaji vya wabunifu mbali mbali wa ndani na nje ya Tanzania.
Asia Idorous alisema kuwa, SFW 2013, ni onesho la aina yake kwani limeweza kuibua wabunifu chipukizi na kuwathamini kwa kazi zao huku likiwa ni kielelezo kwa Tanzania ikiwemo kuvuka hadi nchi jirani. “Ni fursa ya kipekee kwa mimi kuonesha mavazi yangu kwenye SFW 2013, kwani naamini uwepo wangu utakuwa ni somo na funzo kwa wabunfu wengine wanaochipukia kujifunza zaidi” alisema Asia Idorous.
Na kuongeza kuwa, wadau wa tasnia hiyo ya mavazi na mitindo watapata kuona kazi zake mbali mbali alizozibuni kwa ustadi mkubwa katika kipindi hiki cha kumaliza mwaka.
Aidha, aliwataka wabunifu wanaochipukia kulitumia vizuri SFW 2013, kwani hadi kufia hapo limeweza kuibua wabunifu wengi wakiwemo wanaofanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.
Awali Meneja maboresho wa SFW, Hamis Omary alisema onyesho hilo litakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014.
Maonesho hayo yalianza Desemba 5 na kutarajia kumalizika Desemba 8, ambapo wabunifu wanaochipukia na wakongwe wanaonesha mavazi yao ya ubunifu sambamba na wabunifu zaidi ya 15, kutoka nchi tofauti za ndani ya Bara la Afrika na nje..
Tamasha hilo limedhaminiwa na ; EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd, 361 Degrees na Vodacom Tanzania.
ZAIDI ya wabunifu 15 wa kimataifa kuonesha mavazi yao
Swahili Fashion Week 2013 inayoanza usiku wa leo Ijumaa Desemba 6, zaidi ya wabunifu 15 wa kimataifa kuonesha mavazi yao.
Wabunifu hao wanatoka kwenye nchini 9 wakiwa pamoja na wabunifu 27 wa Tanzania watakaonesha nguo mbalimbali zitakazovaliwa mwaka 2014 Afrika Mashariki.
Wabunifu watakaoonesha mavazi yao Ijumaa ni pamoja na Cynthia Schiming – Namibia, Yvonne Ndawana – Zimbabwe, Afrostreet Kollektion – Kenya na Michelle Ouma – Kenya. Siku ya pili (7th Dec 2013) watakaoonesha ni pamoja na Kutowa Designs –Zambia, Walove – Kenya, Lulu Philista Oniang’o – Kenya, Terrance Chipembere –Zimbabwe, Carla Silva – Angola, 2Heads by Atsu – Ghana, Estelle Mantel Clothing – Zambia, Chizika – Czech Republic, Taati Sibolile Maison – Namibia na Palse South Africa – South Africa.
Siku ya tatu (8th Dec 2013) watakaonesha mavazi ni Arapapa by Santa Anzo – Uganda, Hafeni Frans – Namibia, MO Creations & Couture – Zambia, Suhaa Schmitz – Rwanda na David Tlale – South Africa
Kwa upande wa Tanzania wabunifu wa mavazi watakaonesha mkusanyiko wa nguo zao ni pamoja na H &A Dress to Impress, Tanzania Mitindo House, Anne Kiwia Dar es Salaam, Na Kadhalika, Can Wear and Handmade from Tanzania, Malleni Designs, House of Wellu, Keramiti, Catherine Mlowe, Jasmine Greca Sinare, Lucky Creations na Ailinda Sawe
Siku ya pili watakuwepo Martin Kadinda, Hameed Abdul, Khadija Mwanamboka, Dominick Godfrey, Yechi & Yuchi, PSJ Couture na Mgece Makory
Siku ya tatu watakaokuwepo ni Eve Collections, An Nisa Abayas, Eskado Bird, Kiki’s Fashion, Asia Idarous Khamsin, Gabriel Mollel, Zaidi Africa, na Jamilla Vera Swai
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)